Boti
ya polisi iliyokuwa katika doria mashariki ya mkoa wa kusini Unguja
eneo la Jambiani imegonga, mwamba na kusababisha askari waliokuwemo
kutoswa baharini huku mmoja akifariki na mwengine hajaonekana.
Akizungumza
na waandishi wa habari kamishna mkuu wa jeshi la polisi CP Hamdan Omar
Makame amesema boti hiyo inayoitwa ushirikiano ilikuwa katika doria ya
kawaida na ndipo ilipokutana na dhoruba hiyo na ilikuwa na askari sita
ambao mmoja wao akiwa ni afisa wa KMKM na wanne waliweza kuokolewa
nammoja kufariki ambaye ni Said Hassan Saleh na hadi sasa kikosi cha
polisi cha baharini kianendelea kumtafuta afisa wa Polisi Asp Tenga
Seleamn Pandu bado hajaonekana na juhudi zinaendelea kumtafuta.
Akizungumzia
silaha zilizokuwandani ya boti hiyo ambayo ni miongoni mwa boti
zilizotolewa msaada na serikali ya Marekani CP Hamdan Omar Makame
amesema silaha zote zimepatikana naziko salama na hali ya boti hiyo iko
salama na inatarajiwa kuletwa makao makuu ya kitengo cha baharini ili
ichunguzwe.
0 comments:
Post a Comment