HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz - MUSIC HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz: MUSIC - All Post
Showing posts with label MUSIC. Show all posts
Showing posts with label MUSIC. Show all posts

Sentensi 3 za Profesa Jay siku ikitokea kakutana na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete…!

Sentensi 3 za Profesa Jay siku ikitokea kakutana na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete…!
Prof-JayIkiwa imebaki miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika kwa Tanzania,staa wa muziki wa Bongo Fleva ambaye amedumu kwa zaidi ya miaka 15 mtu mzima Profesa Jay anayo ya kusema na Rais Jakaya Kikwete.
Profesa Jay kwenye Exclusive na Amplifaya ametoa sentensi 3 ambazo kama akikutana na Rais leo angemwambia,sentensi ya kwanza amesema kuwa angemwambia Rais awe na maamuzi magumu kwa sababu kama tunachukia Rushwa na ufisadi basi na yeye awe mkali,atumie madaraka aliyonayo kwa sababu anaamini ana uwezo wa kuirudisha Tanzania kwenye mstari.
Sentensi yake ya pili  amesema angemwambia asicheke na Nyani kwani ndio maana anaona tunavuna mabua na huku akimsifia kwa kumwambia mheshimiwa unafanya kazi yako vizuri lakini wanaokuangusha ni watu waliokuzunguka.
Sentensi ya tatu ya Profesa Jay kwenda kwa Rais Kikwete amesema angemwambia Rais awe mkali zaidi atumie nafasi yake kama Rais ili Rushwa na Ufisadi vimalizike ili tuweze kuona matunda ya Tanzania.

WAKALI HAWA KUTIKISA PASAKA DAR LIVE KESHO

WAKALI HAWA KUTIKISA PASAKA DAR LIVE KESHO
HATIMAYE! Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki wengi wa burudani imewadia ambapo kesho Aprili, 5 (Sikukuu ya Pasaka) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar mastaa wa muziki Bongo kama, Ali Kiba ‘Mwana Dar Live’, Isha Mashauzi pamoja na Msaga Sumu wanatarajiwa kutikisa.
Ali Kiba akiupagawisha umati wa Dar Live
Akizungumza na Mikito Nusunusu, mratibu wa burudani katika ukumbi huo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ alianza kwa kuwaomba mashabiki wote kufika kwa wingi kujionea mastaa hao wakifanya maajabu jukwaani.
“Moto wa burudani utawaka kesho hivyo niwaombe tena, siku ya kesho si ya kukosa kutokana na burudani tulizowaandalia,” alisema Abby Cool.
ALI KIBA
Ikumbukwe kuwa tangu mwaka 2013, Ali Kiba hajafanya shoo yoyote katika ukumbi huo na kwa mara nyingine anakuja kama Mwana Dar Live kutokana na wimbo wake unaotikisa kwa sasa wa Mwana.
“Kwa mara ya kwanza Dar Live, Ali Kiba ataimba nyimbo zake live kwa kutumia vyombo na hii itakuwa mwanzo mwisho hivyo itakuwa burudani ya aina yake.
“Kikubwa kitakachoamsha shangwe kwa mashabiki ni staili yake mpya atakayoizindua ya Chekecha Cheketua inayotokana na wimbo wake wenye jina hilohilo huku akiwa na madensa wake wapya.”
Mbali na kuwepo kwa sapraizi kibao hiyo kesho, mashabiki pia wajiandae kuonjeshwa ngoma zinazobamba alizofanya na mdogo wake wakiwa kama Kiba Square ambazo ni Kidela, Pita Mbele na nyingine nyingi.
Kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan 'Isha Mashauzi', akiwapa raha mashabiki ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
ISHA MASHAUZI
Kiongozi wa kundi la muziki wa Pwani, Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ‘Jike la Simba’ naye atakuwepo kesho kuwapa burudani mashabiki wote wa muziki huo.“Kwa mara ya kwanza Isha atautambulisha wimbo wake wa Nimpe Nani huku Mashauzi Classic wakiwakonga kwa nyimbo zao kali kama Ropokeni Yanawahusu , Ni Mapenzi Tu, Tupendane, Bonge la Bwana na nyingine nyingi.”
Mashauzi pia watatoa sapraizi kubwa ikiwa ni pamoja na kuachia nyimbo zao tatu kwa mpigo ambazo ni Tuacheni Tulale, Mapenzi Yamenivuruga pamoja na Wema Hauwezi.
Msanii wa nyimbo za bongo fleva anayetamba na wimbo wake wa 'Nimempata', Pamela Daffa ‘Pam D’.
PAM D Burudani pia itafunikwa na msanii anayekuja kwa kasi, Pamela Daffa ‘Pam D’ ambapo kesho anatarajiwa kutoa shoo ya aina yake akiwa sambamba na madensa wake.Pam D atawabamba na ngoma yake ya Nimempata aliyoshirikiana na Mesen Selekta ambayo ni habari ya mjini kwa sasa.
Kiongozi wa Kundi la Sarakasi la Masai Warriors, MC Darada akielezea kundi lao lilivyojipanga kunogesha shoo ya Mwana Dar Live.
MASAI WARRIORS
Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na kundi maarufu la Masai Warriors ambalo litatoa burudani kibao kwa watoto kama vile kucheza na magunia, sarakasi, yoga, kuimba, kugawa zawadi na vingine vingi.
“Niwaombe tu wazazi wawaruhusu watoto wao kuja sehemu hii muhimu kwa burudani za kijanja. Tumewaandalia pia michezo mingi kama vile ya kubembea, kuteleza,kuogelea na kila mmoja atahakikisha anarudi na zawadi nyumbani kemkemu,” alisema Abby.
Msaga Sumu naye kuuwasha moto Dar Live kesho.
MSAGA SUMU
Pazia la burudani kwa watu wakubwa litafunguliwa usiku ambapo kwa watu wote watakaofika mapema watapata fursa ya kupiga picha ‘red carpet’ na mastaa wote watakaofika kesho sambamba na kuongea nao machache.
“Kwa mara ya kwanza atazindua nyimbo zake tatu kwa mpigo ambazo ni Marafiki Gani, Shemeji Unanitega pamoja na Kidole Changu.”

Lady Jaydee wametoa kibao kipya kwa jina 'MOYO' akishirikiana na Msanii wa Kenya, Atemi

Msanii wa Kenya, Atemi na mwanamuziki wa Tanzania Lady Jaydee wametoa kibao kipya kwa jina 'MOYO'.
'Moyo' ni wimbo kuhusu mapenzi ya matukio tofauti .
Katika wimbo huu Atemi anasema kuwa haijalishi penzi lina mvuto wa kiasi gani mwishowe bado linasalia kuwa penzi.

Wimbo huo uliotungwa na Atemi Oyungu ni 'single' ya kwanza kutoka album yake mpya ya tatu.
Wimbo huo umeandaliwa na R-kay ambaye pia aliandaa wimbo mwengine wa Atemi 'Usijali' akiimba na Delvin Savara wa Sauti Sol.

-BBC

Ni zamu ya Shetta sasa hivi, na hii ndio video yake mpya kamshirikisha Mnigeria.

Shetta 1Ni zamu ya Shetta ambae ni mkali wa bongofleva aliekaa kimya bila kutoa chochote kipya kwa zaidi ya miezi 7 na sasa amerudi kwenye headlines na hii kolabo kampa shavu Kcee wa Nigeria

G Nako na ishu ya kutoza HELA kwenye collabo, kuingia kwenye uigizaji..

G Nako na ishu ya kutoza HELA kwenye collabo, kuingia kwenye uigizaji..
.
.
Rapper wa kundi la Weusi, G Nako amezungumzia kuhusu na kuendelea kuwatoza fedha wasanii wanaomshirikisha katika nyimbo zao pamoja na ishu ya kuingia kwenye filamu.
“Uamuzi wa kuwatoza fedha wasanii katika nyimbo zao wanazonishirikisha bado unaendelea ,unajua muziki wetu unapanuka na watu wengi wanaujua kwa hiyo lazima sasa hivi tuwe katika level za kimataifa..  japokuwa bado katika stage ya kuwaweka watu sawa wasiwe wageni sana na hiki kitu kwa sababu unaweza ukatoka kama msanii kwenda nchi nyingine ukashangaa lakini sio kitu cha kushangaa.. ni kitu cha kawaida kabisa..“– G Nako
Mbali na kutoza fedha wasanii katika nyimbo anazoshirikishwa, kagusia pia kuhusiana na kuingia kwenye uigizaji; “Unajua kwenye sanaa kuna mahusiano  kati ya vitu viwili ambazo ni muziki na filamu kwa hiyo mashabiki wasishangee kuniona kwenye TV. Kuna short clips nimeigiza kwenye hiyo series ila bado haijatoka, tuko kwenye maandalizi ya kuelekea kumalizia“–alisema G Nako.

Diamond na Linex wamekutana tena, hizi ni picha walivyotengeneza video yao kijijini jana







Flora Mbasha: Hizo Stori Mnazosikia Hazina Ukweli Wowote na ndio Maana Niliamua Kukaa Kimyaa

" Hizo stori mnazosikia hazina ukweli wowote na
ndio maana niliamua kukaa kimya sikutaka
kujibizana kwenye vyombo vya habari kwa uongo
wa baadhi ya magazeti ya udaku ila ninasikitika
sana kwani kuna watu wamekaa na kujipanga
kisawa sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanaharibu
huduma yangu kwa gharama zozote, lakini bado
ninasonga mbele kwani mwanzilishi wa huduma
yangu ni Mungu na huyo ndiye atakayeimaliza na
sio mwanadamu "
Hayo alifunguka mwimbaji wa nyimbo za injili
Flora Mbasha

DIAMOND PLATNUMZ AMJIBU KWA VITENDO MPENZI WA ZAMANI WA ZARI

DIAMOND PLATNUMZ AMJIBU KWA VITENDO MPENZI WA ZAMANI WA ZARI

Diamond akiwa kwenye baiskeli huku Zari akiwa kwenye BMW X6.

Baadhi ya post za King Lawrence Instagram akimkejeli Diamond.
STAA wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameamua kumjibu kwa vitendo anayedai kuwa aliwahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King Lawrence ambaye amekuwa akimtupia maneno ya kumtusi na kejeli mitandaoniBaadhi ya post za King Lawrence Instagram akimkejeli Diamond.
STAA wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameamua kumjibu kwa vitendo anayedai kuwa aliwahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King Lawrence ambaye amekuwa akimtupia maneno ya kumtusi na kejeli mitandaoni.
Diamond akipozi na mpenzi wake Zari.
King Lawrence ambaye ni binamu wa aliyekuwa mume wa Zari aliyezaa naye watoto watatu Ivan amekuwa akimnanga Diamond mitandaoni hasa Instagram kama mtu aliyefulia na hana fedha ambapo siku za nyuma aliwahi kuandika post akisema kuwa yuko tayari kumpatia kiasi cha Usd 40,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 71 Diamond aachane na Zari.

Diamond akiwa kwenye baiskeli huku Zari akiwa kwenye BMW X6.
Baadhi ya post za King Lawrence Instagram akimkejeli Diamond.
STAA wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameamua kumjibu kwa vitendo anayedai kuwa aliwahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King Lawrence ambaye amekuwa akimtupia maneno ya kumtusi na kejeli mitandaoni.
Diamond akipozi na mpenzi wake Zari.
King Lawrence ambaye ni binamu wa aliyekuwa mume wa Zari aliyezaa naye watoto watatu Ivan amekuwa akimnanga Diamond mitandaoni hasa Instagram kama mtu aliyefulia na hana fedha ambapo siku za nyuma aliwahi kuandika post akisema kuwa yuko tayari kumpatia kiasi cha Usd 40,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 71 Diamond aachane na Zari.
Katika kuonyesha kuchoshwa na tabia hizo za King Lawrence, Diamond ameamua kutupia picha yake akiwa amepanda baiskeli huku mpenzi wake Zari akiwa katika mkoko mkali aina ya BMW X6 akimaanisha kumkebehi mtu huyo kuonyesha kuwa hana kitu ila anaomba penzi kwa mtoto mkali aliye kwenye B

KUWA WA KWANZA KUTAZAMA VIDEO MPYA YA DAVIDO "THE SOUND"....NI KALI MBAYAAAA!!!!

. 


Staa wa Nigeria David Adedeji Adeleke aka Davido time amekuletea video ya single mpya inayoitwa The Sound akiwa amewashirikisha Dj Buckzpamoja na kundi la Uhuru kutokaea Afrika Kusini.


Itazame hapa #The Sound bonyeza play

DIAMOND PLATINUMZ, RAIS JK SIRI NZITO!


Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.
NYUMA ya ukaribu wa Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, kuna siri nzito kufuatia mambo mbalimbali yanayojitokeza kati yao kila kukicha, Amani lina cha kukujuza.
Katika kuunga maelezo hayo, inasemekana kwamba mbali na mambo mengine, hivi karibuni Diamond alimpelekea JK tuzo zake tano za kimataifa alizotwaa mwaka 2014 kwa kuwa nyuma yake kulikuwa na sapoti kubwa ya mkuu huyo wa nchi. 
UKARIBU MKUBWAKwa mujibu wa chanzo cha karibu ambacho ni ‘mtu’ wa Diamond, staa huyo amekuwa ‘klozdi’ sana na JK kufuatia mambo yake mengi ya msingi kuyafanya kwa kumshirikisha, kiasi kwamba kuna wakati Diamond hata akikurupuka usiku wa manane kama ana jambo huwa hasiti kumpigia simu mheshimiwa na kuongea kwa muda huku wakicheka weee!

Kundi la muziki P-Unit kutoka Kenya ladaiwa kusambaratika ikiwa ni miaka saba toka waungane.

Kundi la muziki P-Unit kutoka Kenya ladaiwa kusambaratika ikiwa ni miaka saba toka waungane.
P-unit

Kwa mujibu wa Standard Digital, members wa kundi hilo lililozaliwa mwaka 2007, kila mmoja ameanza kufanya solo project.
Frasha anatarajiwa kuzindua project yake binafsi Ijumaa hii, huku Gabu na Bon Eye wakifuata mkondo huo pia.
P-Unit ambao ni washindi wa tuzo za Channel O, walifanikiwa kutoa album yao ya kwanza “Wagenge Hao” mwaka 2010 ambayo ilibeba hits kama ‘Kare’, ‘Una’ (featuring DNA), ‘Hapa Kule’, ‘Kushoto Kulia’ and ‘Si Lazima’, ambazo zilifanya vizuri na kukuza jina lao Afrika Mashariki.
Kundi lingine la muziki Kenya lililosambaratika miaka ya karibuni ni Camp Mulla, ambao nao pia kila mmoja wao sasa anafanya muziki kama solo.
Source: SDE

DIAMOND PLATNUMZ KUFANYA MAKAMUZI KATIKA UTOAJI TUZO ZA MWANASOKA BORA WA AFRIKA NCHINI NIGERIA LEO

DIAMOND PLATNUMZ KUFANYA MAKAMUZI KATIKA UTOAJI TUZO ZA MWANASOKA BORA WA AFRIKA NCHINI NIGERIA LEO

Diamond Platnumz akifurahia jambo na mmoja wa wasanii wa Kundi la P Square, Peter Okoye wakati akijiandaa kwa ajili ya shoo yake ya leo nchini Nigeria.
Diamond akibadilishana mawazo na mwanamuziki Fally Ipupa jijini Lagos.
MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' leo atakinukisha katika sherehe za utoaji tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2014.
Zoezi hilo litafanyika leo Januari 8, 2015 jijini Lagos nchini Nigeria kuanzia majira ya saa 3 usiku.
Wakali wengine watakaokuwepo kutoa burudani leo ni pamoja na P Square, Flavour, Uhuru, Fally Ipupa na wengineo.

DIAMOND ATEULIWA KUTUMBUIZA TUZO ZA MWANASOKA BORA CAF

Na Saleh Jembe
Msani Nasib Abdul ‘Diamond’ amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye hafla ya utoaji tuzo za mwanasoka bora Afrika 2014. Diamond atatumbuiza katika tuzo hizo ambazo wachezaji 25 nyota barani Afrika wamechaguliwa kugombea tuzo hizo. Hafla hiyo itafanyika Januari 8, 2015 jijini Lagosi Nigeria. Mwanasoka Bora, Yaya Toure raia wa Ivory anayeitumikia Manchester City ya England ni kati ya watakaowania nafasi hiyo. 

Wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika:

1.    Ahmed Musa                          (Nigeria, CSKA Moscow)
2.    Asamoah Gyan                       (Ghana, Al Ain)
3.    Dame N’doye                         (Senegal, Lokomotiv Moscow)
4.    Emmanuel Adebayor               (Togo, Tottenham)
5.    Eric Maxim Choupo-Moting          (Cameroon, Schalke 04)
6.    Fakhreddine Ben Youssef            (Tunisia, CS Sfaxien)
7.    Ferdjani Sassi                          (Tunisia, CS Sfaxien)
8.    Yao Kouassi Gervais ‘Gervinho’ (Cote d’Ivoire, AS Roma)
9.    Islam Slimani                          (Algeria, Sporting Lisbon)
10. Kwadwo Asamoah                   (Ghana, Juventus)
11. Mehdi Benatia                         (Morocco, Bayern Munich)
12. Mohamed El Neny                   (Egypt, Basel)
13. Pierre-Emerick Aubameyang        (Gabon, Borussia Dortmund)
14. Raïs M'Bolhi                           (Algeria, Philadelphia Union)
15. Sadio Mané                            (Senegal, Southampton)
16. Seydou Kieta                          (Mali, As Roma)
17. Sofiane Feghouli                     (Algeria, Valencia)
18. Stephane Mbia                       (Cameroon,  Sevilla)
19. Thulani Serero                        (South Africa, Ajax)
20. Vincent Aboubakar                  (Cameroon, Porto)
21. Vincent Enyeama                    (Nigeria, Lille)
22. Wilfried Bony                          (Cote d’Ivoire, Swansea)
23. Yacine Brahimi                       (Algeria, Porto)
24. Yannick Bolasie                       (DR Congo, Crystal Palace)
25. Yaya Toure                            (Cote d’Ivoire, Man City)

Wanaowania tuzo za Mwanasoka Bora Afrika( Kwa wachezaji wanaocheza Afrika)

1.    Amr Gamal                     (Egypt, Al Ahly)
2.    Abdelrahman Fetori          (Libya, Ahly Benghazi)
3.    Bernard Parker               (South Africa, Kaizer Chiefs)
4.    Bongani Ndulula               (South Africa, Amazulu)
5.    Akram Djahnit                 (Algeria, ES Setif)
6.    Ejike Uzoenyi                   (Nigeria, Enugu Rangers)
7.    El Hedi Belamieri              (Algeria, ES Setif)
8.    Fakhereddine Ben Youssef   (Tunisia, CS Sfaxien)
9.    Ferdjani Sassi                    (Tunisia, CS Sfaxien)
10. Firmin Mubel Ndombe          (DR Congo, AS Vita)
11. Geoffrey Massa                  (Uganda, Pretoria University)
12. Jean Kasusula                     (DR Congo, TP Mazembe)
13. Kader Bidimbou                  (Congo, AC Leopards)
14. Lema Mabidi                       (DR Congo, As Vita)
15. Mudathir Al Taieb                (Sudan, Al Hilal)
16. Roger Assalé                     (Cote d’Ivoire, Sewe Sport)
17. Senzo Meyiwa                    (South Africa, Orlando Pirates)
18. Solomon Asante                 (Ghana, TP Mazembe)
19. Souleymane Moussa            (Cameroon, Coton Sport)
20. Yunus Sentamu                  (Uganda, AS Vita)

Msama azungumzia "kuachana" na Rose Muhando, Akanusha Rose Muhando kutumia Madawa ya Kulevya



Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ametamka kuwa yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa waimbaji wengine.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msama kwa vyombo vya habari juzi, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote wa muziki wa Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokana na nafasi yake katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15.

Msama, mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na kuandaa matukio ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na Tamasha la Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ambayo amekuwa akipata juu ya Rose.

“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayomualika na kushindwa kutokea.
 
“Lakini, naomba watumishi wa Mungu wanielewe katika hili, sipokei mialiko wala simzuii Rose. Mimi ninapokuwa na matamasha, nimekuwa nikimualika kama wafanyavyo wengine.
 
“Nimekuwa nikimlipa kiasi cha fedha anachotaka na hakuna zaidi, hivyo mimi sio Meneja wake,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza:
 
“Agosti mwaka huu, kampuni yangu ilidhamini uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu, haikuwa na maana kwamba ni Meneja wake.

“Nilimualika uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu Oktoba mwaka huu, nilimlipa fedha, lakini hakutokea kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wengine ambao wamekuwa wakilalamikia tabia hiyo,” alisema Msama.
 
“Pia wiki iliyopita nilikuwa na Tamasha la Krismasi tulikubaliana aje katika maonesho hayo, lakini hakutokea na tulishamlipa,”alisema Msama kwa masikitiko na kuongeza kuwa amemsamehe na anamuombea kwa Mungu aweze kubadilika.

Alieleza kuwa hana tatizo na mwimbaji huyo, wala hana ugomvi naye, lakini amekuwa akipata taabu kutoka kwa baadhi ya wachungaji pale Rose anapoalikwa halafu hatokei na inaonekana yeye ndiye amemzuia.

“Sijawahi kupokea mialiko kwa niaba ya Rose, kila kitu anafanya mwenyewe, hivyo ni vyema wadau wakafahamu hilo,” alisema Msama na kusema angekuwa mwepesi wa kulalamika, angeshafanya hivyo muda mrefu dhidi ya Rose.

Aidha, Msama amekana kuhusiana na madai ya Rose kutumia dawa za kulevya na kusisitiza kuwa hajawahi kumuona akijidunga kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti na kuongeza kama ikiwa ni kweli, hilo pia ni suala binafsi.

“Baadhi ya vyombo vya habari vinaandika ni mjamzito, nafikiri pia hayo ni mambo yake binafsi na hakuna mtu mwenye haki au uhalali wa kuhoji hilo.Yule ni mtu mzima na mwenye kujielewa,” alisema Msama.

Rose ni mwimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini aliyejipatia sifa ndani na nje ya ukanda wa Afrika Mashariki ambaye mwishoni mwa mwaka 2013, alisaini mkatabawa kufanya kazi na kampuni ya muziki ya Sony ya Afrika Kusini.

Miongoni mwa albamu zilizompa umaarufu Rose kiasi cha kuwa alama ya mafanikio ya muziki wa injili nchini, ni ‘Uwe Macho,’ Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, ‘Mungu Anacheka’ na Wololo na Kamata Pindo la Yesu aliyoachia hivyo karibuni.

ROSE MHANDO ATUMBUIZA NA KITUMBO

Mwanamuziki ‘grade one’ wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando akitumbuiza.

BAADA ya kudaiwa kulipwa fedha na kuingia mitini kwenye matamasha mbalimbali, mwanamuziki ‘grade one’ wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando (pichani) amenaswa akitumbuiza jukwaani akiwa na ujauzito mkubwa.
Tukio hilo lililowashangaza watu wengi lilitokea Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Ilongero jimbo la Singida Kaskazini kulipokuwa na mkutano wa hadhara aliokuwa akiuhutubia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Wakati wananchi wakimsubiri Nyalandu ambaye pia ni mbunge wa Singida Kaskazini ahutubie, zilitangulia burudani za hapa na pale ndipo baadaye alipopanda Rose akiwa na kitumbo ‘ndii’ na kusababisha minong’ono chini kwa chini.
“Mh! Jamani huyu ni Rose kweli au macho yangu? Si angepumzika? Mbona tumbo tayari kubwa hivi, hata kama ni kusaka pesa lakini si kwa staili hii, kuna wakati mtu inabidi fedha uzipe kisogo,” alisikika mmoja wa wananchi. 
Hata hivyo sambamba na watu kutilia shaka juu ya afya yake, Rose alionekana kulimudu vyema jukwaa kwa kutumbuiza nyimbo zake huku akiimba kwa staili ya kurukaruka kama kawaida.
Kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Ilongero na jimbo zima la Singida Kaskazini, mbali na kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo, Nyalandu alitangaza nia ya kugombea urais mwakani.

Rose Muhando awa tapeli sugu...apokea pesa za kufanya show bila ya kutokea akiogopa kuonekana na mimba jukwaani

Rose Muhando awa tapeli sugu...apokea pesa za kufanya show bila ya kutokea akiogopa kuonekana na mimba jukwaani
Habari zilizoenea kwenye magazeti na mitandao ni kwamba Muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando safari hii amemtapeliAlex Msama baada ya kupokea fedha kwa makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo hakutokea!

“Hii ni mara ya pili, kwenye uzinduzi wa albamu ya msanii John Lisu pale Diamond Jubilee (Dar), Rose alipokea shilingi milioni moja kutoka kwa Msama lakini siku ya uzinduzi hakutokea. Kusema ukweli huu utapeli wa Rose wa kuchukua fedha za watu halafu hatokei sasa imekuwa too much. Nimesikia habari kwamba ameogopa kutokea uwanjani hapa ambako tamasha lilifanyika kwa kuhofia mimba yake kuonekana maana kwa sasa ni kubwa.” Kimesema chanzo hicho cha habari

Una lipi la kumwambia Rose juu ya jambo hili? na unalizungumziaje jambo hili?

Muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando safari hii amemtapeli Alex Msama baada ya kupokea fedha kwa makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo hakutokea!
“Hii ni mara ya pili, kwenye uzinduzi wa albamu ya msanii John Lisu pale Diamond Jubilee (Dar), Rose alipokea shilingi milioni moja kutoka kwa Msama lakini siku ya uzinduzi hakutokea. Kusema ukweli huu utapeli wa Rose wa kuchukua fedha za watu halafu hatokei sasa imekuwa too much. Nimesikia habari kwamba ameogopa kutokea uwanjani hapa ambako tamasha lilifanyika kwa kuhofia mimba yake kuonekana maana kwa sasa ni kubwa.” Kimesema chanzo hicho cha habari
Una lipi la kumwambia Rose juu ya jambo hili? 



je unalizungumziaje jambo hili?

Diamond, Mzee Yusuph kwenye usiku wa Wafalme Dar Live… Idris na Samantha wa #BBAHotshots ndani (Picha)

Diamond, Mzee Yusuph kwenye usiku wa Wafalme Dar Live… Idris na Samantha wa #BBAHotshots ndani (Picha)

.
.
Christmas ya mwaka 2014 itabakia kuwa na historia kubwa kwenye dunia ya burudani, 88.5 usiku wa Dec 25 wamepokea shangwe za burudani kutoka kwa Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na Mzee Yusuph kwenye  viwanja vya Dar Live, Mbagala Dar es Salaam.
Burudani ilikuwa kubwa zaidi kwa kuwa kwa mara ya kwanza yule mshindi wa #BBAHotshots Idris Sultan alitokezea kwenye stage yenye watu wengi zaidi akiwa ameongoza na Samantha ambaye walishiriki wote mashindano hayo.
Kama uliikosa hiyo, hapa kuna picha, mwanzo mpaka mwisho ya Usiku wa Wafalme pale Dar Live.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC_0478
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.