IMEFICHUKA! Mrembo
wa Uganda ambaye kwa sasa ndiye ‘usingizi’ wa Mbongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ hivi karibuni alitua Bongo na
kulala nyumbani kwa mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’, Sinza-Mori
jijini Dar.
Mrembo wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’.
Chanzo makini kilicho karibu na familia
ya Diamond kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Zari alipata fursa ya kupiga
‘mbonji’ nyumbani hapo alipomtembelea Diamond.
“Alikuja akambonji kwa mama Diamond kama
siku mbili hivi halafu wakaondoka wote wakati Diamond alipokwenda
Nigeria kwenye shoo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2014.
Kikizidi kumwaga data, chanzo kilisema, mbali na kulala, Zari alishiriki kazi za ndani ikiwemo kupika na kupakua kama ilivyokuwa kwa zilipendwa wa Diamond, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo hakutaka kufafanua mengi zaidi ya kukiri kwamba mrembo huyo alikuja Dar na kuondoka naye.
Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa na 'Diamond Platnumz'.
“Wewe jua alikuja, nikaondoka naye hayo mambo mengine siwezi kuyazungumzia,” alisema Diamond.
Amani lilipomtafuta mama Diamond kwa njia ya simu hakupatikana lakini mtu wa karibu alisema kwa sasa hatumii simu kwa sababu ambazo hazikutajwa.
Amani lilipomtafuta mama Diamond kwa njia ya simu hakupatikana lakini mtu wa karibu alisema kwa sasa hatumii simu kwa sababu ambazo hazikutajwa.
0 comments:
Post a Comment