Meseji ya Wolper Yatibua Uchumba wa Nay wa Mitego | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

Meseji ya Wolper Yatibua Uchumba wa Nay wa Mitego



Mwigizaji Jacqueline Wolper ameibua tafrani la aina yake kwa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kumtumia meseji iliyomtia shaka mpenzi wa staa huyo, Siwema. 
 
Tukio hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Nay wa Mitego, Kimara- Korogwe jijini Dar  ambapo ilisemekana Wolper alituma SMS iliyokuwa ikiuliza muafaka wa jambo fulani ndipo Siwema akaja juu na kuanza kumcharukia bebi wake huyo.

Alipoulizwa Nay wa Mitego kuhusiana na ugomvi huo, alifunguka:
“Wolper ni rafiki yangu kitambo, ni mtu wangu tunayeelewana kupita maelezo, hivyo juzikati nilikuwa nikichati naye juu ya kutaka kumshirikisha kwenye video ya wimbo wangu mpya wa Akadumba, Siwema dizaini kama alimaindi kuona nawasiliana naye lakini nilimuelewesha na kila kitu kipo sawa.”
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment