Amri
imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na karibu
abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki
kwenda Italia.
Abiria
waliokuwa kweye ferry hiyo walipiga simu kwa vituo vya runinga nchini
Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na upepo unatatiza shughuli za
uokoaji.
Maafisa
wa ulinzi wa pwani nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman
Atlantic ilikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati
walipotuma ujumbe.
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari.
chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment