HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz - HAZARDS HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz: HAZARDS - All Post
Showing posts with label HAZARDS. Show all posts
Showing posts with label HAZARDS. Show all posts

Breaking News: Watu 10 Wafariki Dunia Baada ya Basi la kampuni ya Unique Kugongana na Gari la Coca Cola


Habari  zilizotufikia  zinaarifu  kuwa  basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.

Watu 10 wamefariki na  50 wamejeruhiwa.Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.






BUS CRASH TO KILL 19 PEOPLE TODAY IN MBEYABUS CRASH TO KILL 19 PEOPLE TODAY IN MBEYA


Imeua bus accident 19 people prominent location as Airport, Kiwila, Mbeya region after the bus that plunged into the river.
News from the scene zinaarifu that only two people have been recovered, including the conductor. 
This accident occurred after Coaster performing his travels between Mbeya and Kyela bus boycott that some urban decide to carry passengers.




Breaking news: moto mkubwa wateketeza jengo la hostel ya mabibo...wanafunzi waunguliwa na vitu vya thamani


Habari zilizotufikia hivi punde moto mkubwa umezuka katika moja ya jengo lililopo Katika hostel za mabibo ambayo yanamilikiwa na kuendeshwa na chuo kikuu Dar es salaam ... Askari wa zima moto walichelewa kufika ambapo imesababisha hasara kubwa kwa wanafunzi kwa kuunguliwa vitu vyao vya thamani mbalimbali. Moto huo umezuka katika ghorifa ya juu.mpaka sasa jitihada za kuuzima moto huo zinaendelea.

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoishi kwenye Hostel za Mabibo,wakiangalia moja ya majengo ya Hostel hizo likiwalimeshika moto asubuhi hii.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na msaada wa haraka unahitajia ili kuokoa mali zilizopo kwenye Jengo hilo.
Hakuna anaeamini anachokiona,kwani imekuwa ni tukio la ghafla sana.
Baadhi ya Wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye Jengo hilo wakiwa nje,huku wakiwa hawajui la kufanya wakati moto huo ukiendelea kuwaka.
Moshi unazidi kufuka na moto unaongezek

BREAKING NEWS: ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo baada ya kupata ajari mbaya

BREAKING NEWS: ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo baada ya kupata ajari mbaya
   
ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia
moja wamefariki dunia mkoani Singida leo,

baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina
ya Noah T.730 BUK, kugongwa na Lori aina ya Scania.
Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa
1.32 asubuhi katika barabara kuu ya
Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna
tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani
Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya
kuja Singida mjini.
Amesema hadi sasa miili ya abiria 10
wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye
chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida

Majina ya Abiria Wote Wa Ajali Ya Basi Iliyoua Watu 42 Mafinga Yako Hapa

"Ni ajali ambayo haijawahi kutokea katika maeneo haya," ni baadhi ya maneno yaliyosikika kutoka kwa wakazi wengi wa mjini Mafinga na vitongoji vyake, ambao jana walishuhudia ajali  katika historia ya mji huo.
Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company lililokuwa likiendeshwa na Maka Sebastian (26)  na basi aina ya Scania namba T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa likiendeshwa na Baraka Gabriel (38).
  Wakati lori lilikuwa likielekea Barabara ya Mafinga-Mbeya, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
  Ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 42 wakiwemo 40 waliokuwemo katika basi na wawili katika lori hilo, ilitokea katika eneo la Changarawe takribani kilometa 5 kutoka mjini Mafinga, mkoani Iringa, katika barabara kuu ya Mafinga-Mbeya.
  Kati ya waliokufa yupo dereva wa basi hilo, huku dereva wa lori akijeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa na kitu kama nondo shingoni mwake.
Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Asas na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, Mungi alisema ajali hiyo ilitokea jana asubuhi saa tatu na nusu.
  Kamanda Mungi alisema jeshi lake kwa kushirikiana na hospitali za Mafinga na Mkoa wa Iringa wanaendelea kutambua majina ya watu waliokufa na  majeruhi.
  Kamanda Mungi alisema taarifa zao za awali zinaonesha chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa barabara. Mungi alisema lori na basi hilo yaligongana uso kwa uso wakati madereva wake wakishindana kuwahi kuchepuka moja kati ya mashimo makubwa yaliyopo pembezoni na katikati mwa barabara hiyo katika eneo hilo.
  Baadhi ya watu waliotajwa kuwepo katika basi na lori hilo ambao hata hivyo hawakuweza kufahamika mara moja, nani kafa na nani kajeruhiwa ni pamoja na Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni na Frank Chiwango.
  Wengine ni Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine, Mwajengo, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri.
  Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge na Juma Sindu.
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.
  Habari kutoka Mbeya zinaeleza kuwa wakati basi hilo linaondoka kituoni abiria waliokuwepo kwenye basi hilo walikuwa ni 37 ambao ni: 
  Baraka Ndone  ambaye ni dereva, Yahya  Hassan ambaye ni kondakta, Esther    Emmanuel, Henry Lugano, Lusekelo Enock, Jeremia  Watson, Hamad, Olga Solomon, Neto, Theresia Kaminyoge, Frank Chiwanga, Luteni Sanga, Alfred Sanga, Doto Katunga,  Juliana Bukuku, Esther Fidel,  Paulina Josia.
  Wengine ni Iman Mahenge,  Catherine Mwate, Mathias Justine,  Rebeka Kasambala,  Upendo William, Mbamba Ipyana,  Ndulile Kasambala, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule, Mustafa Ramadhani,  Musa, Omega Mwakasege, Shadra Msigwa, Lucy Mtanga, Charles Mweisonga, Martin Haule, Dominick Mashauri, Kelvin Ebadi, Juma Saidi,  na Nicko

Nini Chanzo cha Usagaji kwa Wanawake Bongo ?

Heshima kwenu mabibi na mabwana.
Nimekua nikijiuliza mara kwa mara kuhusiana na suala la usagaji kwa wasichana bila kupata jibu stahiki.
Baadhi ya wasichana wanadai kwamba kuachwa na wapenzi wao mara kwa mara kunachangia kwa kiasi kikubwa wao kujiingiza katika mapenzi ya jinsia moja,
wengine wanadai kwamba shule za boarding zinawasababishia kujiingiza katika mambo haya kwani muda mwingi wanakua wao wenyewe tu bila kujichanganya na wavulana.
Nini maoni yako wewe mwanajamvi,karibuni wakinadada muweze kutupa ukweli wa hili jambo,wavulana pia mnaruhusiwa kuchangia chochote ili tupate mawazo tofauti tofauti.
Asanten

Wagombea urais wapigana vikumbo kwa Komba


KIFO cha Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kepteni John Komba (CCM), kimewafanya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaotajwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, kupigana vikumbo huku kila mmoja akizungumzia umuhimu wa kiongozi huyo.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria msiba nyumbani kwa marehemu, Mbezi kwa Komba jijini Dar es Salaam ni pamoja Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.


Wengine ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa.


LOWASSA
Akizungumzia msiba huo, Lowassa alisema ni pigo kwa taifa, CCM na kwake binafsi.


Alisema kuwa, Komba alikuwa mhamasishaji na mpiganaji aliyetaka CCM iendelee kushika dola.


“Kuondoka kwa Komba ni pigo kwa taifa, chama na kwangu binafsi. Taarifa za kifo hiki nilizipata nikiwa njiani natoka Monduli, nilisikitika sana. Kifo hiki kinatupa funzo, kwamba Mungu akitaka, utake usitake, lazima uondoke,” alisema Lowassa.


NGELEJA
Kwa upande wake, Ngeleja ambaye pia ni Mbunge wa Sengerema (CCM), alisema wamepoteza mtu wa kazi na aliyesimamia mambo aliyokuwa akiyaamini.


Alisema kwamba, Komba alikuwa kiongozi wa kujitolea kwa wananchi na kufundisha uzalendo wa kupenda nchi kwa kupitia nyimbo zake.


“Watanzania tumemkosa mzalendo na tumekosa masomo yake kupitia sanaa. Lakini, natoa rai kwa Serikali kuendelea kuwaenzi na kuwaendeleza wasanii,” alisema Ngeleja.


Alisema funzo aliloliacha Kepteni Komba ni kuwajali wanyonge na kuwatumikia wananchi Watanzania.


MEMBE
Naye akizungumzia kifo hicho, alisema msiba huo umegusa ukanda mzima wa Afrika Mashariki kutokana na umaarufu wa marehemu aliokuwa nao katika sanaa enzi za uhai wake.


“Alipata umaarufu tangu akiwa Chuo cha Ualimu Marangu kule Moshi na baadaye alipokuwa jeshini ambako Mosses Nnaye aligundua sauti yake na kumshawishi kuingia CCM,” alisema.


Membe alimwelezea marehemu Komba kama alikuwa ishara ya upendo, ushirikiano na mshikamano.


“Kifo chake ni kama mshumaa uliozima ghafla, kwani kwa chama alikuwa na nguvu ya kukipa ushindi, hivyo tunamuomba Mungu atupe mshumaa mwingine wa kuendeleza alipoachia Komba.


“Taifa limempoteza mbunge mkweli asiye mnafiki, kitaifa alihusika kuwa shahidi wa kuonyesha mipaka ya Ziwa Nyasa kuwa sehemu ya Tanzania kwa kuonyesha makaburi ya babu zake yaliyopembeni mwa ziwa hilo,” alisema.


MWIGULU
Kutokana na kifo hicho, Mwigulu alisema Kepteni Komba alikuwa ni mtu aliyetengeneza nembo ya CCM na pia ameondoka katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu ambacho alikuwa akihitajika zaidi.


Alisema kwamba, alizungumza na marehemu Jumapili iliyopita ambako alimgusia kuhusu maendeleo ya jimbo lake la Mbinga Magharibi.


“Nilimtania kwamba katika nyimbo zako usiache kutaja jina langu, akanitania kwamba jina lako linaimbika. Jambo ambalo sitasahau ni nyimbo zake kuzitumia katika magari ya matangazo zilizosaidia kujaza watu katika mikutano,” alisema.


Dk. Asha-Rose Migiro
Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, alisema kifo cha mwanasiasa huyo ni pigo kwa CCM na wabunge wengine pia.


“Nakumbuka siku mbili kabla ya kifo chake, nilikutana naye na akanihakikishia kwamba atapita kwa kishindo Oktoba jimboni mwake.


“Huyu alikuwa kiunganishi cha taifa katika matukio, kwa mfano lile la kifo cha Mwalimu Nyerere kwa kupitia nyimbo zake,” alisema Dk. Migiro.


DK SLAA
Wakati hao wakisema hayo, Dk. Slaa alisema kila mtu atakuwa ameguswa na kifo cha Kepteni Komba kwa kuwa alikuwa akijulikana zaidi na wakati mwingine kuwazidi baadhi ya viongozi wa kitaifa.


“Kifo hicho ni pigo, hasa kwa chama chake cha CCM ambacho alikuwa mhamamishaji wake na pia ni pigo kwetu kwa kuwa inatukumbusha kuwa kila mtu ataondoka na imani yangu ni kwamba, atakuwa ameondoka salama kama tulivyoelezwa na wasemaji wengi hapa,” alisema Dk. Slaa.


Pamoja na hayo, alitoa wito kwa Watanzania kuungana kumuombea marehemu ili afike salama na kuelekea mahali pema na salama.


PROFESA LIPUMBA
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kifo cha Kapteni Komba ni pigo kwa CCM na hata kwa Watanzania kwa kuwa alikuwa na mchango mkubwa.


“Kwanza natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wa Mbinga Magharibi na CCM kwa kuondokewa na mtu muhimu. Kapteni Komba alikuwa mwanasiasa, mwanasanaa na alitoa mchango mkubwa.


“Alihamasisha wananchi kukipigia kura CCM kutokana na nyimbo zake. Kwa kipindi hiki sisi wapinzani tunaungana na wenzetu wa CCM kwa sababu kifo kinamkuta mtu yeyote.


“Nyimbo zake zimependwa si tu na wanachama wa CCM, lakini pia na Watanzania kwa ujumla,” alisema Profesa Lipumba.


MAKINDA
Spika wa Bunge, Anne Makinda, alitoa siri kwamba ndiye aliyemshauri Komba kugombea ubunge mwaka 2005 katika Jimbo la Mbinga Magharibi.


“Nilipokutana naye katika awamu ya pili ya uongozi wa Rais Mkapa, aliniambia nia yake ya kugombea ubunge mwaka 2010, nikamkatalia na kumshauri agombee 2005 na akafanikiwa kupata ubunge,” alisema.


NAPE
Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema amempoteza mtu muhimu kwake ambaye alikuwa baba na mhamasishaji wa chama.


“Komba kwangu ni baba kwa sababu baba yangu, Moses Nnauye ndiye alishiriki kumshawishi kutoka Jeshi la Wananchi na kujiunga na CCM,” alisema.


Akizungumzia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Nape alisema anaamini TOT itakuwa imara kwa kuwa Kateni Komba alikuwa amewajenga vijana wadogo.


“Msiba huu umeahirisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana mkoani Dodoma na sasa inatarajiwa kuendelea keshokutwa,” alisema.


Khadija Kopa
Naye mwimbaji wa muda mrefu wa Bendi ya TOT aliyokuwa akiiongoza Kapteni Komba, Khadija Kopa, alimuelezea marehemu huyo kuwa alikuwa ni miongoni mwa watu waliompatia ujasiri alionao hivi sasa.


“Bila ya kunichukua kwa ushawishi wa Moses Nnauye kutoka Zanzibar ambako nilikuwa nikifanya kazi katika Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), leo nisingepata umaarufu huu,” alisema Kopa.


Msemaji awa mbogo
Wakati huo huo, taarifa zilizokuwa zimeenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha mwanasiasa huyo, zilimfanya Katibu wa Bendi ya TOT, Gasper Tumaini, kuwa mbogo na kushangazwa na hoja zinazoibuliwa kuhusu mali za marehemu na kifo chake.


Alisema taarifa za kupigwa mnada kwa nyumba za marehemu si sahihi, kwani siku kadhaa chache zilizopita, Kapteni Komba alikuwa akiugua ugonjwa wa shinikizo la damu pamoja na kisukari.
“Habari hizo zimekuwepo kwa muda mrefu na wala hazikuwa na ukweli wowote zaidi ya kwamba amefariki kutokana na maradhi ya shinikizo la damu na kisukari,” alisema.


Alisema kwamba, marehemu Komba alifariki akiwa katika mipango ya kustaafu muziki, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.


“Jumapili iliyopita alikuwa akifanya mazoezi ya wimbo wake mpya ambao alitarajia kuutoa hivi karibuni, baada ya kutoa wimbo ulioanza kutamba unaoitwa CCM ni ile ile’,” alisema.


Andrew Komba
Mtoto mkubwa wa marehemu Komba, Andrew Komba, alisema kama familia wamepata pigo kubwa kwa kuwa ndiye alikuwa akiunganisha familia na alijenga misingi ya kupendana na kusaidiana.


Ratiba ya mazishi
Akitoa ratiba ya mazishi, Msemaji wa Familia hiyo, Dominic Mwakangale, alisema itakuwa imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni chama na Bunge.


Alisema kuwa, jana mwili wa marehemu ulitolewa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam saa 10 jioni na kupelekwa kanisani kwa ajili ya maombezi. Leo saa nne asubuhi, mwili huo utaagwa katika Viwanja vya Karimjee.


Baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo, alisema mwili wa marehemu utachukuliwa na kupelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Songea kwa ajili ya mazishi.


KIFO
Kapteni Komba alifariki juzi jioni ambapo taarifa iliyotolewa na Hospitali ta TMJ alikokuwa akipatiwa matibabu, zilieleza kuwa alifariki dunia kwa ugonjwa wa shinikizo la damu na kisukari.

Moto wateketeza maduka ya wafanya biashara jijini Tanga

Moto wateketeza maduka ya wafanya biashara jijini Tanga


Maduka ya wafanyabiashara mbali mbali yaliyopo mtaa wa india jijini Tanga yameteketea kwa moto kwa kile kinachodaiwa kuwa imetokana na hitilafu ya umeme.

Moto huo uliokuwa ukifukuta ndani katika maeneo hayo ya biashara ulisababisha baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo kutaka kulishambulia gari la zima moto la halmshauri ya jiji la Tanga kufuatia kufika katika eneo la tukio lakini wakati linaaza zoezi hilo ghafla likaishiwa na maji katika kipindi cha dk 3 na kuamsha hasira kwa mamia ya wananchi.
Hata hivyo akielezea hatua hiyo kamanda wa opesheni wa kikosi cha zima moto mkoani tanga Bwana Kumenya Bakari amekemea vikali jazba za wananchi za kushambulia mara kwa mara gari la zima moto la halmashauri ya jiji  la tanga na kufafanua kuwa wanapofika katika eneo la tukio jambo la kwanza wanaanza kwanaza kuokoa maisha ya watu,mali ndio kisha baadae kuzima moto katika eneo husika.

BREAKING NEWS: MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MEZ B AFARIKI DUNIA HIVI PUNDE


Msanii mez b amefariki dunia leo hii baada ya kuugua... Taarifa za kuaminika kutoka kwa dada yake anayeitwa Rachel kuwa marehemu mez b amefariki akiwa kwao Dodoma .
Tutawaletea habari zaidi za msiba..

PICHA ZA AJALI ILIYOTOKEA IRINGA NA KUUA WATATU NA PIKIPIKI KUWAKA MOTO

Hizi ndivyo lori hilo lilivyoharibika
WATU watatu waliokuwa wamepakizana mishikaki wamekufa kwa kuteketea kwa moto mjini Iringa usiku huu baada ya usafiri aina ya pikipiki (Boda boda)waliyokuwa wakisafiri kutoka mjini Iringa kuelekea Nduli nje kidogo na mji wa Iringa kugongana na lori aina ya fusu na kupelekea pikipiki hiyo kuwaka moto.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya Lori na boda boda leo usiku 

Hii ndio pikipiki iliyoteketea kwa moto baada ya ajali 
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 usiku huu wakati boda boda hiyo ikiwa katika mwendo mkali kugongana na lori hilo ambalo pia lilikuwa katika mwendo na kusababisha vifo hivyo . 
Mashuhuda wamesema kuwa kijana mmoja ambae inasadikika ndie dereva wa boda boda hiyo ametambuliwa kwa jina moja la Julius huku wengine wawili bado kutambuliwa . 
Kutokana na ajali hiyo mbali lori hilo upande wa mbele ngao yake ilipinda huku eneo hilo la mbele likiharibika vibaya mfano wa kugongana gari kwa gari na baada ya hapo pikipiki hiyo ilishika moto na kuteketea yote pamoja na watu hao ambao miili yao ilizimwa kwa mchanga na wasamaria wema.
Miili ya marehemu hayo imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa utambuzi zaidi

MEYA MANISPAA MOROGORO NA WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI - MSAMVU

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( wa kwanza kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro , Said Amanzi , wakipita eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.
Gari la Meya likiwa halitamaniki.
Wasamalia wakimuwahisha Hospital,Mmoja wa majeruhi mara baada ya kupata ajali eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .
Hili ndilo basi lililogongana na Gari ya Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo ,(45) akiwa amelazwa wodi namba tano ya daraja la kwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari yake SM 4151 ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam ,mbali na Meya huyo na watu wengine watatu ,Dereva Mwambala Ally (55), na waandishi wa habari , Anita Chali (30) pamoja na HUSSEIN Nuha (28) pia walijeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu. 
Mwandishi wa habari,Anita Chali akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari waliyoipata,walipokuwa kwenye kazi na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akionesha eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kupimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.


MEYA wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro , Amir Nondo (45), dereva  na waandishi  wa habari wawili wamepata ajali   baada ya  gari walilokuwa wakisafiria kugongwa na basi la abiria lenye namba za usajili T 831 CEH, aina ya Scania mali ya kampuni ya Happy Africa na kujeruhiwa  sehemu mbalimbali za miili yao na kulazwa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Tukio hilo lilitokea Januari 30, mwaka huu majira ya saa 9: 30 alasiri , eneo la Msamvu Mzambarauni darajani katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam, ambapo basi hilo lilikuwa likotokea mkoani Njombe.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo akisaidiwa na baadhi ya Madiwani wa Manispaa hiyo alipofikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kupata ajali eneo la Mzambarauni Darajani. Gari lake liligongana na Basi la Happy Africa lililokuwa likitokea Njombe kuelekea Dar es Salaam katika barabara kuu ya Dar es Salaam jana
Majina ya watu hao wengine waliojeruhiwa na kulaza katika wodi za daraja la kwanza katika hospitali ya rufaa ya mkoa , ni dereva wa gari la Meya, Mwambala Ally (55) , na waandishi wa habari ambao ni wapigapicha vituo vya televisheni , Anitha Chali (30) pamoja na Hussein Nuha (28).

Mstahiki meya huyo  aliyekuwa kwenye gari ya Halmashauri ya Manispaa hiyo  yenye namba za usajili SM 4151, ikiendeshwa na Mwambala  ambamo pia walikuwemo waandishi wa habari hayo na alikuwa katika msafara wa ziara ya kikazi ya mkuu wa mkoa huo,Dk Rajab Rutengwe.

Meya Nondo akizungumzia  ajali hiyo, akiwa wodini akipatiwa matibabu  ,sambamba na majeruhi wengine alisema baada ya kufika eneo la Mizambarauni, Darajani, lilichomoka pembeni basi la abiria ililokuwa likitokea Njombe kuelekea  Dar es  salaam, na kuligonga kwa mbele gari alilokuwemo.

Mashuhuda wa ajali hiyo  waliwaambia waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio,  kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni basi la abiria mali ya kampuni ya Happy Africa, kuingilia msafara huo wa mkuu wa mkoa uliokuwa ukielea mjini baada ya kukagua shughuli za ujenzi wa vyumba vya maabara na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Bigwa katika  Shule ya Sekondari Sumaye.

Mkuu wa mkoa kwa takribani wiki mbili amekuwa katika ziara katik halmashauri saba za mkoa huo kwa ajili ya kukagua shughuli za ujenzi na umaliziaji wa maabara tatu kwa kila shule ya skondari ya Kata na pia kutumia fursa hiyo kujitambulisha , kusikiliza kero na kuzipatia majawabu ya msingi.

Januari 29 na 30 mwaka huu ilikuwa ni zamu ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Shule ya sekondari Sumaye kilikuwa ni kituo chake cha mwisho katika ziara hiyo na baadaye kufanyika kwa majumuisho ya ziara hiyo Januari 31, mwaka huu mjini Morogoro.

Hata hivyo baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya mkoa , viongozi mbalimbali walifika kuwajulia hali  wakati wakiendelea kupatia matubabu na madaktari mbingwa wa hospitali hiyo, akiwemo Mganga mkuu wa mkoa , Godfrey Mtei.

Mstahiki Meya Nondo ameumia sehemu ya kichani na mkononi , wakati na mpiga picha Anita Chali, ameumia  kichwani, huku dereva pamoja na  Hussein wakiumia zaidi  kwenye paji la uso na kichwani huku Hussein akisaidiwa na mashine ya kupumulia (oxygen).

 Kufuatia tukio hilo Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa imesema itatoa taarifa ya ajali hiyo  jumamosi ya  Januari  31, mwaka huu.

AJALI MBAYA YATOKEA KOROGWE NA KUUA WATU WATATU PAPO HAPO



 AJALI hii mbaya ilitokea juzi (Jumapili) katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambapo watu watatu wanadaiwa kupoteza maisha.
 Dereva wa gari hili lililopata ajali amelazwa katika Hospitali ya KCMC, Moshi akiendelea na matibabu.CHANZO GPL

HIVI NDIVYO MHESHIMIWA SUGU ALIVYOUMIA BAADA YA KUPATA AJALI JANA KITONGA

Mr. Sugu akiwa Hospitali.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali hiyo imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa mchana wa leo.kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa Mh. Mbilinyi alikuwa safarini akitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar akiwa na jamaa zake Wanne katika gari hilo lenye namba za usajili T 148 BQE. katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Gari linavyoonekana kwa karibu.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.


Gari hiyo inavyoonekana.