HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz - HOME HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz: HOME - All Post
Showing posts with label HOME. Show all posts
Showing posts with label HOME. Show all posts

Mashambulizi kwa wageni Afrika Kusini bado ni ishu kubwa, hii ni ripoti nyingine kutoka huko (VIDEO)

Xenophobia-In-South-Africa-Nigerians-Victims-650x398
Stori ya ishu ya ubaguzi Afrika ikarudishwa kwenye headlines na matukio ya South Africa.. Xenophobia ikachukua nafasi ya ripoti nyingi za habari kubwa Afrika kwa zaidi ya mwezi mmoja, kwa sasa hivi ni kama hali imetulia japo sio kwa asilimia 100 !!
Wenyeji wanahofu kuendelea kuwepo Afrika Kusini, hii imeripotiwa na kituo cha TV  cha SABC Afrika Kusini, wageni wengine 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliamua kuanza safari ya kurudi kwao ikiwemo Wamalawi.
Watu zaidi ya 100 walilazimika kurudi kwenye nchi zao kutokana na kuanza kwa vurugu za mashambulizi ya wenyeji wa South Africa waliokuwa wakiwafukuza wageni.. wengine waliuawa na wapo waliojeruhiwa na kupoteza mali zao pia kutokana na mashambulizi hayo.
“Nataka nirudi nyumbani kwa sababu huku hali sio nzuri.. wanatupiga, wanataka kutuua nimeona nirudi tu nyumbani“– Hassan Shalifa, mmoja ya raia wa kigeni waliokuwa wakijiandaa kuondoka South Africa.

KAMANDA MKUU WA BOKO HARAMU AUAWA, NGOME YAO YASAMBALATISHWA

KAMANDA MKUU WA BOKO HARAMU AUAWA, NGOME YAO YASAMBALATISHWA
Meja Jenerali Chris Olukolade.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa, vikosi vya nchi hiyo vimemuua kamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.

Meja Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa, Abu Mojahid kamanda wa ngazi za juu wa kundi la Boko Haram ameuawa katika mapigano kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria ameongeza kuwa, wapiganaji kadhaa wa Boko Haram wameuawa pia katika mapigano yanayoendelea kati ya jeshi na wanamgambo hao.

Wakati huo huo taarifa kutoka Nigeria zinasema kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuukomboa msitu wa Sambisa ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya kundi la kigaidi la Boko Haram.

Msitu wa Sambisa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria uko umbali wa karibu kilomita 100 kutoka Chibok mji ambao mnamo mwaka mmoja uliopita kundi la Boko Haram liliteka nyara zaidi ya wasichana 200 wa shule na kuwapeleka kusikojulikana.

Hayo yanajiri katika hali ambayo operesheni ya pamoja ya vikosi vya Nigeria, Chad, Cameroon na Niger dhidi ya Boko Haram inaendelea huku kukiwa na taarifa kwamba, imekuwa na mafanikio

VIDEO: AJIYEJIFICHA FEMALE STUDENT IN A CUPBOARD FOR 48 HOURS DURING THE ATTACK OF THE UNIVERSITY OF GARISSA EATING 'LOTION' ASIMULIA STUDY WHOLE



Female student who was hiding in a cupboard for 48 hours during the attack of the University of Garissa in Kenya finally has jitokeza.Msichana he says that spent fuel type 'lotion' as food in order to live. 

If your device KINAUWEZO Click PLAY VIDEO BELOW AND Listen AKISIMULIA Study WHOLE happened on KILLINGS


 

PICHAZ za hali ilivyokuwa UBUNGO leo APRIL 10 2015

 PICHAZ za hali ilivyokuwa UBUNGO leo APRIL 10 2015
Vurugu kubwa zimezuka, yakachomwa matairi ya magari barabarani.. hakuna basi lolote la abiria kwenda mikoani lililokuwa limetoka wala hakuna daladala iliyokuwa ikipakia abiria katika eneo hilo.
Baada ya kuanza vurugu Polisi waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya.
AW1A1328
AW1A1329
AW1A1332
AW1A1333
AW1A1336

AW1A1344
AW1A1346
AW1A1350
Muonekano wa stendi ya mabasi Ubungo kwa juu, hakuna gari hata moja ambayo ilisafiri kwenda Mikoani leo.

AW1A1352
AW1A1356
AW1A1359
Barabarani hazionekani gari za abiria, watu wanatembea kwa miguu.

DSC_0001
DSC_0002
DSC_0003
DSC_0012
DSC_0015
DSC_0017
DSC_0020
DSC_0021
DSC_0023
Wengine walizuia hata gari za watu binafsi kuonekana ikipakia abiria yoyote.

DSC_0025
AW1A1271
Baadi ya maeneo usafiri ni bodaboda, Noah na magari binafsi. Wengine wanatembea kwa miguu.
AW1A1275
Askari Polisi wakitoa matairi wa magari yaliyowekwa Ubungo

AW1A1278
AW1A1281
AW1A1284
AW1A1289
AW1A1292
AW1A1295
Kuna baadhi ya watu waliokamatwa kwa kuhusika na vurugu hizo

AW1A1307
Gari la Polisi likitoa matairi yaliyowekwa barabarani na kuchomwa moto.

AW1A1309
AW1A1314
AW1A1316
AW1A1317
AW1A1320
AW1A1322
AW1A1324
AW1A1327
AW1A1332
Madereva hao wamegoma kutokana na sababu mbalimbali, mojawapo ni shu ya utaratibu wa kutakiwa kwenda Chuoni kusoma tena baada ya muda wa leseni zao kuisha

CBE YAENDESHA UTAFITI KUWASAIDIA MACHINGA KUTAMBULIWA RASMI

CBE YAENDESHA UTAFITI KUWASAIDIA MACHINGA KUTAMBULIWA RASMI
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam  Prof. Emanuel Mjema (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu utafiti  wa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) unaofanywa na chuo hicho kwa kushirikiana  na  Shirika la Wafanyabiashara  kutoka nchini  Finland (FBMA)  kwa lengo la kubaini  fursa za biashara zilizopo , faida, changamoto  na mchango wao katika maendeleo ya taifa pindi watakapoingizwa kwenye mfumo rasmi unaotambulika kisheria.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam  Prof.  Simon Msanjila (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu  mchango wa utafiti  wa shughuli za wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) unaofanywa na chuo hicho kwa kushirikiana  na  Shirika la Wafanyabiashara  kutoka nchini  Finland (FBMA) utakavyochangia maendeleo ya sekta ya biashara nchini.
Na Aron Msigwa – MAELEZO
9/4/2015, Dar es Salaam
Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwa kushirikiana  na  Shirika la Wafanyabiashara  kutoka nchini  Finland (FBMA)  kinafanya utafiti  wa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) kwa lengo la kubaini  fursa za biashara zilizopo , faida, changamoto  na mchango wao katika maendeleo ya taifa pindi watakapoingizwa kwenye mfumo rasmi unaotambulika kisheria. 
Akizungumzia utafiti huo leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema amesema kuwa kwa kipindi kirefu wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga wamekuwa katika malumbano na mamlaka za miji na majiji kote nchini kutokana na kukosa mfumo rasmi unaotambua biashara zao.
Amesema chuo chake kwa kuliona jambo hilo kikishirikiana na Shirika la Wafanyabiashara wa Finland (FBMA) kimeamua kuendesha utafiti huo kuanzia mwaka 2014 na kuongeza  kuwa matokeo ya awali yaliyopatikana ndani ya mwaka mmoja yamebainisha kuwa jiji la Dar es salaam lina wamachinga zaidi ya Laki saba (700,000) wanaofanyabiashara zao nje ya mfumo rasmi unaotambulika kisheria.
“Katika utafiti tumegundua kuwa Dar es salaam ina wamachinga wengi zaidi kuliko maeneo mengine walio nje ya mfumo rasmi unaotambuliwa na Serikali hii ni fursa, kwa sasa hakuna mfumo wowote unaotambua uwepo wao na baadhi yao wamekuwa wakilumbana na vyombo vya usalama na mamlaka husika jambo lililojenga uadui miongoni mwao” Amesema Prof. Mjema.
Amesema katika kutatua changamoto hizo utafiti huo utaangalia jinsi gani wamachinga watatambulika kisheria katika mfumo rasmi , pia kukisaidia Chuo cha Elimu ya Biashara kuandaa mitaala na programu mbalimbali za masomo ya biashara kwa vijana hao ambao wengi wao wameishia elimu ya darasa la 7 ili kuwajenge uwezo wa kutunza kumbukumbu za biashara zao pamoja na kuiwezesha Serikali kuweka utaratibu wa wafanyabiashara hao kufikiwa na huduma muhimu katika maeneo yao.
Aidha, amesema utafiti huo utawasaidia wafanyabiashara hao kuepuka hasara wanayoipata mara kwa mara kutokana na bidhaa zao kukamatwa na wakati mwingine kuharibiwa na mamlaka zinazohusika wakati wa oparesheni mbalimbali za kuwaondoa katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria kufanya biashara.
“Katika utafiti huu tunapendekeza kuanzishwa kwa mfumo rasmi wa kuwatambua  wamachinga wote kote nchini ili waweze kujulikana  na  shughuli wanazofanya na  mchango wao kwa taifa” Amesisitiza.
Katika hatua nyingine Prof. Emanuel Mjema amesema kuwa chuo chake kiko katika hatua za mwisho za uanzishaji wa mafunzo ya Shahada ya Ualimu katika Biashara  ili kuziba pengo la uhaba wa walimu wa kufundisha masomo ya Biashara katika shule za Sekondari na vyuo kote nchini.
Amesema chuo chake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kimefikia uamuzi huo kufuatia  utafiti uliofanywa na jopo la wataalamu wa maandalizi ya Mtaala wa kufundishia programu hiyo mwaka 2012  uliobaini uwepo wa kiwango kikubwa cha uhitaji wa waataalam wa kufundisha masomo ya biashara wenye taaluma ya ualimu.
“Sisi kama chuo cha Elimu ya Biashara tumeona uhitaji uliopo nchini wa kukosa wataalam wa kufundisha masomo ya Biashara wenye taaaluma ya ualimu ndio maana tumeamua kuanzisha  mtaala huu wa kufundishia wanafunzi wa Shahada ya Elimu katika Biashara ili  tupate wahitimu bora watakaofundisha wanafunzi wetu na kukidhi mahitaji ya soko” Amesisitiza.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof.Simon Msanjila akifafanua kuhusu  utafiti huo amesema  kuwa Serikali itanufaika zaidi kutokana na kutambua mchango wa wafanyabiashara hao pindi itakapowaingiza katika mfumo rasmi.
Amesema wafanyabiashara hao wanapotembeza bidhaa zao barabarani, mitaani pamoja na maeneo mbalimbali ya miji hufanikiwa kusanya zaidi ya shilingi elfu thelathini kwa siku ( 30,000) jambo linalotia matumaini  kwa sekta ya biashara na Serikali iwapo watathaminiwa na kujengewa mazingira mazuri ya kutambuliwa

BREAKING NEWS: MGOMO WA MADEREVA WAANZA ASUBUHI YA LEO SEHEMU MBALIMBALI NCHINI


Mgomo  wa  Madereva  umeanza  rasmi  leo  katika  maeneo  mbalimbali   nchini kama ambavyo muungano wa madereva wa vyombo vya usafiri waliahidi wakidai kutotatuliwa kero zao na serikali.
Sababu  kubwa  ya  madereva  hao  kugoma  ni  kuishinikiza  serikali  kuweka  mfumo  mzuri  wa  ajira  na  kupinga  kanuni  inayowataka  kurudia  kusoma  katika  chuo  cha  taifa  cha  usafirishaji,NIT  kila  leseni  zao  zinapokwisha  muda. 
Madereva  hao  wanadai  malalamiko  yao  makubwa  ni  kitendo  cha  Serikali  kuongeza  kifungu  kidogo  katika  sheria  mpya  ya  mwaka  2015  namba 31  inayowataka  madereva  wote  wenye  leseni  za  madaraja  E,C1,C2,C3  na  C kurudi  darasani  kila  baada  ya  miaka  mitatu  kuongeza  utaalamu  katika  fani  hiyo  ya  udereva  ili  kupunguza  ajali  za  mara  kwa  mara  zinazotokea. 
 
Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.