KAMANDA MKUU WA BOKO HARAMU AUAWA, NGOME YAO YASAMBALATISHWA | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

KAMANDA MKUU WA BOKO HARAMU AUAWA, NGOME YAO YASAMBALATISHWA

Meja Jenerali Chris Olukolade.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa, vikosi vya nchi hiyo vimemuua kamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.

Meja Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa, Abu Mojahid kamanda wa ngazi za juu wa kundi la Boko Haram ameuawa katika mapigano kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria ameongeza kuwa, wapiganaji kadhaa wa Boko Haram wameuawa pia katika mapigano yanayoendelea kati ya jeshi na wanamgambo hao.

Wakati huo huo taarifa kutoka Nigeria zinasema kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuukomboa msitu wa Sambisa ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya kundi la kigaidi la Boko Haram.

Msitu wa Sambisa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria uko umbali wa karibu kilomita 100 kutoka Chibok mji ambao mnamo mwaka mmoja uliopita kundi la Boko Haram liliteka nyara zaidi ya wasichana 200 wa shule na kuwapeleka kusikojulikana.

Hayo yanajiri katika hali ambayo operesheni ya pamoja ya vikosi vya Nigeria, Chad, Cameroon na Niger dhidi ya Boko Haram inaendelea huku kukiwa na taarifa kwamba, imekuwa na mafanikio
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. Casinos Near You - Jackson Casino Resort & Spa
    The 강원도 출장샵 closest 양산 출장마사지 casinos to you can get close 동두천 출장마사지 to you 양산 출장샵 include the Ak-Chin Indian Village & the River City Casino & Hotel, 의정부 출장마사지 a favorite on the strip.

    ReplyDelete