JINA Zari hivi sasa limekuwa jina maarufu katika masikio ya Watanzania, Afrika Mashariki na kwingineko hasa baada ya mwanadada huyo mfanyabiashara na mwanamuziki wa Uganda kuwa na urafiki na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassib Abdul maarufu kwa jina la usanii Diamond Platnum.
Kwenye
mitandao ya kijamii kama Tweeter, Facebook, Instagram na hata Whatsapp
lazima utakutana na jina Zari akiunganishwa na Diamond na wengine
wataunganisha na Wema Sepetu aliyewahi kuwa mpenzi wa Diamond.
Uhusiano
kati ya Zari na Diamond umezua gumzo kila eneo Tanzania na Afrika
Mashariki huku wakifananishwa na mastaa wa nje kama vile Kanye West na
Kim Kardashian kwa namna wanavyofuatana wakati wote huku Diamond
akionesha kila aina ya mbwembwe za kumjali mrembo huyo kutoka Kampala,
Uganda.
Uhusiano
wa Zari na Diamond umewafanya kuandamana kila sehemu hivi sasa. Wawili
hao walianza kuonekana kuwa na ukaribu wa mahusiano tangu Diamond
alipokwenda Afrika Kusini kwenye Tuzo za Channel O ambapo Diamond
aliibuka na ushindi wa Tuzo tatu.
Baada
ya Tuzo hizo, Zari alimualika Diamond kushiriki katika ‘pati’ maarufu
ambayo mwanadada huyo huandaa kila mwaka nchini Uganda ambapo mwaka huu
ilijulikana kama All White Ciroc Party.
Wawili
hao baada ya sherehe hiyo, walifuatana ambapo Zari alimsindikiza
Diamond nchini Rwanda na Burundi alipokwenda kutoa burudani nchini humo,
na picha kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kuwafanya wawili hao
kuwa gumzo hivi sasa katika mitandao Tanzania na Afrika Mashariki. Je,
Zari ni nani hasa?
Zarina Hassan Tlale,maarufu kama Zari ni Mganda anayeishi Afrika Kusini. Mrembo huyo ni mwanamuziki na mfanyabiashara. Ni mwanamke aliyefanikiwa na anayependa kuishi maisha ya kifahari. Anamiliki magari ya kifahari na yenye gharama kubwa kama Lamborghini Gallardo, BMW- 2006, Chrysler-2008, Audi Q7-2010 na Ranger Rover Sports.
Zarina Hassan Tlale,maarufu kama Zari ni Mganda anayeishi Afrika Kusini. Mrembo huyo ni mwanamuziki na mfanyabiashara. Ni mwanamke aliyefanikiwa na anayependa kuishi maisha ya kifahari. Anamiliki magari ya kifahari na yenye gharama kubwa kama Lamborghini Gallardo, BMW- 2006, Chrysler-2008, Audi Q7-2010 na Ranger Rover Sports.
Mwanadada
huyo ni binti wa Halima Sultan Hassan na Nasur Hassan akiwa na asili ya
damu mchanganyiko ikiwa ni pamoja na ya Kihindi , Toro, Somalia na
Burundi kutoka mji wa Jinja, Uganda. Babu mzaa mama yake anatoka India
na bibi yake ni kutoka Uganda. Babu yake mzaa baba ni kutoka Somalia na
bibi yake mzaa baba anatoka Burundi.
Zari
maarufu kama The Bosslady aliwahi kuolewa na mwanamume anayejulikana
kwa jina la Ivan na kubarikiwa watoto watatu wa kiume Pinto, Didy na
Quincy na anamiliki kampuni tatu. Mwanadada huyu alizaliwa Septemba 23,
1980. Zari amekulia katika mji wa Jinja katika nchi ya Afrika Mashariki
inayojulikana kama Uganda.
Zari
alisoma shule ya msingi, kisha kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana
ya Jinja ambapo alisoma kwa bidii kutimiza ndoto zake. Baada ya kumaliza
elimu ya sekondari, mwanadada huyo alihamia katika mji mkuu wa nchi
hiyo, Kampala ambapo alikuwa akitoa burudani ya muziki katika maeneo ya
starehe kabla ya kuhamia mjini London, Uingereza na kusomea Stashahada
ya masuala ya urembo (cosmetology).
Historia
yake kimuziki inaonesha Zari alianza kuimba akiwa na umri mdogo wakati
akisoma shule ya msingi ambapo alikuwa akitoa burudani katika matamasha
ya muziki yaliyokuwa yanaandaliwa na wafanyakazi wa shule, wakati wa
hafla za mwishoni mwa mwaka na katika mashindano mengine ya jumuiya
akiwakilisha shule yake.
Ingawa
amekulia katika familia ya Kiislamu yenye wasichana sita na wavulana
wawili, Zari hakuacha mapenzi yake kwenye muziki. Alianza muziki akiwa
na umri mdogo na albamu yake ina nyimbo kali kama ‘Toloba’ na ‘Hotter
Than Them’. Watu waliomvutia katika muziki ni Wasanii wa Marekani
Arethal Franklin na Whitney Houston wakati akiwa sekondari.
Afrika
waliomvutia akapenda muziki ni wanamuziki wa Afrika Kusini Brenda
Fassie, Miriam Makeba, Lucky Dube na Malkia wa Muziki Afrika Kusini,
Yvone Chaka Chaka.
Alipojiunga na sekondari alijiunga na makundi ya dansi, drama na muziki jambo ambalo lilimsaidia kuchaguliwa kwa miaka miwili mfululizo la Muigizaji Bora.
Alipojiunga na sekondari alijiunga na makundi ya dansi, drama na muziki jambo ambalo lilimsaidia kuchaguliwa kwa miaka miwili mfululizo la Muigizaji Bora.
Baada
ya miaka miwili ya kufanya vizuri katika majukwaa na matamasha ya
shule, alipumzika na kuhama kutoka Uganda kwenda London, Uingereza na
kuendelea na masomo yake lakini bado mapenzi yake kwa muziki yakiwa
mawazoni mwake.
Zari kwa msaada wa familia, mashabiki na marafiki wa- naopenda mtindo wa muziki wake na kuamini anaweza aliamua kuchukua hatua mwaka 2007 wa kurekodi singo yake ya kwanza inayoitwa Oliwange (ikiwa na maana wewe ni wangu) .
Zari kwa msaada wa familia, mashabiki na marafiki wa- naopenda mtindo wa muziki wake na kuamini anaweza aliamua kuchukua hatua mwaka 2007 wa kurekodi singo yake ya kwanza inayoitwa Oliwange (ikiwa na maana wewe ni wangu) .
Mwaka
2008 Zari alishinda Tuzo ya Channel O ya Video Bora ya Muziki ya Msanii
Bora Afrika Mshariki. Hafla ya tuzo hizo ilifanyika Johannesburg,
Afrika Kusini. Tangu hapo Zari ameendelea kutoa nyimbo zaidi za kuvutia,
huku akitiwa moyo na mashabiki wake wakati huo.
Mwaka
2009 alipata Tuzo inayojulikana kama Diva ya mwaka katika kipengele cha
Diaspora tangu hapo aliendelea kutengeneza muziki. Zari hivi sasa
anaishi Afrika Kusini ambapo anamiliki maduka makubwa ya vipodozi na
shule ya elimu ya juu mjini Pretoria wakati akiendelea kujijenga
kimuziki.
Inaelezwa
kuwa Zari na aliyekuwa mumewe Ivan wanamiliki Shule ya Brooklyn City
ambayo ina kampasi sita Afrika Kusini, huku kila moja ikiwa na wanafunzi
kati ya 800 hadi 2,100. Wanafunzi hao hupewa vyeti vya taifa
wanapomaliza mwaka. Vile vile Zari amejenga hosteli iliyopo barabara ya
Sir Apollo Kaggwa, Kampala na anamiliki nyumba kadhaa katika mji huo
hasa eneo la Munyonyo, pamoja na duka kubwa la nguo Afrika Kusini.
Ingawa
muziki wake haujafanya vizuri kama wanamuziki wengine wa Uganda akiwemo
Jose Chameleone, Bebe Cool, Bobi Wine na Ragga Dee, Zari amekuwa
akifurahia kwa mafanikio zaidi kwenye biashara na kutokana na hilo
anasema lazima arudishe kwa jamii na hivyo kuamua kusaidia vituo na
taasisi kadhaa zinazohitaji misaada kama Katalemwa Cheshire Home, Sanyu
Babies’ Home pamoja na Gereza la Luzira.
Mfano
mwaka 2013 kutokana na moyo wake wa kusaidia, kwa kutimiza hilo baada
ya sherehe zake anazozifanya kila mwisho wa mwaka aliamua kutembelea
Kituo cha Watoto Yatima cha M-Lisada kilichopo Nsambya siku moja kabla
ya Sikukuu ya Krismasi, akifuatana na watoto wake Pinto, Didy na Quincy.
Alitoa
zawadi maalum kwa watoto hao, ambapo Zari alishiriki kuandaa chakula
cha Krismasi na kisha baadaye kutoa msaada wa vitu kama vile
taulo za wanawake, sukari, biskuti, mchele na matoke. Mbali na masuala
mengine yote, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, watu wengi nchini Uganda
wanakubaliana kuwa Zari ndio Mwanamke Mrembo zaidi nchini humo.
“Sitafuti
umaarufu, wenyewe umaarufu ndio hunifuata,” aliwahi Zari kusema kupitia
mtandao wa Red Pepper akikanusha habari za baadhi ya watu wanaodai kuwa
anatafuta umaarufu kwa nguvu.
0 comments:
Post a Comment