Mehmet Ali Agca aliyetaka kumuua papa John wa Pili mwaka 1981.
Mwanamme mmoja raia wa Uturuki
aliyempiga risasi na nusura amuue aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki
papa John Paul wa pili mwaka 1981 ameweka maua kwenye kaburi lake katika
makao makuu ya kanisa katoliki ya Vatican.
Ziara ya Mehmet Ali Agca kwenye
makao ya Vatican inafanyika miaka 30 tangu John Paul amtembelee gerezani
na kumsamehe kwa kujaribu kumuua.
Bwana Agca aliomba kukutana na kiongozi wa sasa wa kanisa katoliki papa Francis lakini hata hivyo ombi lake lilikataliwa
Aliachiliwa kutoka gerezani
nchini Italia mwaka 2000 na kisha baadaye akatumikia kifungo chengine
cha miaka 10 nchini Uturuki kwa makosa tofauti.
Hadi sasa sababu zake za kutaka kumuua papa John Paul hazijulikani.
chanzo : bbc
0 comments:
Post a Comment