breaking news:Boti ya doria ya Polisi yagonga mwamba mashariki ya mkoa wa kusini Unguja na kusababisha mmoja akifariki na mwengine hajaonekana mpaka sasa | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

breaking news:Boti ya doria ya Polisi yagonga mwamba mashariki ya mkoa wa kusini Unguja na kusababisha mmoja akifariki na mwengine hajaonekana mpaka sasa

Boti ya polisi iliyokuwa katika doria mashariki ya mkoa wa kusini Unguja eneo la Jambiani imegonga, mwamba na kusababisha askari waliokuwemo kutoswa baharini huku mmoja akifariki na mwengine hajaonekana.

Akizungumza na waandishi wa habari kamishna mkuu wa jeshi la polisi CP Hamdan Omar Makame amesema boti hiyo inayoitwa ushirikiano ilikuwa katika doria ya kawaida na ndipo ilipokutana na dhoruba hiyo na ilikuwa na askari sita ambao mmoja wao akiwa ni afisa wa KMKM na wanne waliweza kuokolewa nammoja kufariki ambaye ni Said Hassan Saleh na hadi sasa kikosi cha polisi cha baharini kianendelea kumtafuta afisa wa Polisi Asp Tenga Seleamn Pandu bado hajaonekana na juhudi zinaendelea kumtafuta.


Akizungumzia silaha zilizokuwandani ya boti hiyo ambayo ni miongoni mwa boti zilizotolewa msaada na serikali ya Marekani CP Hamdan Omar Makame amesema silaha zote zimepatikana naziko salama na hali ya boti  hiyo iko salama na inatarajiwa kuletwa makao makuu ya kitengo cha baharini ili ichunguzwe.
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment