Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ akiwa na bebi wake Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
Stori: Waandishi Wetu
JAMBO limezua jambo, saa chache baada ya mwanadada mtafutaji kunako tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kuvalishwa pete ya uchumba na mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ tayari watu wameanza kuisengenya.
JAMBO limezua jambo, saa chache baada ya mwanadada mtafutaji kunako tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kuvalishwa pete ya uchumba na mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ tayari watu wameanza kuisengenya.
Shilole alivalishwa pete hiyo katika sherehe yake ya kuzaliwa
iliyofanyika katika ‘apartment’ za Baraka Plaza, Mikocheni jijini Dar
ambapo mara baada ya mwanadada huyo kukata keki na kuwalisha watu
mbalimbali waliohudhuria, ndipo Nuhu alipomsapraizi mwanadada Shilole
kwa kumvisha pete hiyo.
Kitendo hicho kilionekana kukubalika na waalikwa wengi, lakini wengine
hawakufurahishwa nacho kwa madai eti kwamba Nuhu ni mdogo kuliko
Shilole hivyo hakustahili kuvisha pete mtu mwenye umri kama dada’ke.
“Mh! Mwenzangu hii kali, mimi siku zote Nuhu niliamini hayupo serious
kutembea na Shilole maana ni mkubwa kuliko yeye lakini sasa hapa
kanishangaza kweli, kwa nini asitafute mdogo mwenzake?,” alisikika dada
mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Hata hivyo licha ya masengenyo hayo kusambaa chini kwa chini, Nuhu
aliwakata watu vilimilimi kwa kutamka hadharani kuwa wanapendana na
Shilole hivyo haoni ajabu kama kuna watu hawatakubaliana na penzi lao.
‘Shilole’ akiwa pembeni ya keki yake ya bethidei wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa.
“Tukio linalotendeka hapa limepewa baraka zote na wazazi wetu wameridhia
mimi na mchumba wangu tuoane na hii ni hatua ya kwanza tu mengine
yatafuata na msishangae sana kuona wazazi wetu hawapo eneo hili ni
kwamba wanatambua kinachoendelea hapa.
“Najua wengi mtakuwa na maswali kuhusu hili, mimi na yeye tunapendana na
ndiyo maana leo hii namvisha pete mpenzi wangu na Mungu atatujaalia
katika maisha yetu,” alisema Nuhu na sherehe ikaendelea kwa watu kula na
kunywa.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Steven Mengere
‘Steve Nyerere’, Wellu Sengo ‘Matilda’, Shettah, Martin Kadinda, Mh.
Temba, Chegge, DJ Choka na DJ Tass.
Steve Nyerere aliyekuwa MC wa shughuli hiyo alisema Shilole ni shemeji
yake kwani yeye ni kaka yake Nuhu, na kwamba tukio linalofanyika hapo,
wao kama ndugu wamekubaliana na ndoa itafungwa.
“Siku zote huwa namwambia shemeji yangu kuwa yeye ni mtafutaji kwa hatua aliyofikia mpaka sasa na ninamkubalisana shemeji yangu, karibu Iringa,” alisema muongoza sherehe huyo.
“Siku zote huwa namwambia shemeji yangu kuwa yeye ni mtafutaji kwa hatua aliyofikia mpaka sasa na ninamkubalisana shemeji yangu, karibu Iringa,” alisema muongoza sherehe huyo.
-GPL
0 comments:
Post a Comment