MIMBA YA AUNT EZEKIEL IMEZUA BALAA! | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

MIMBA YA AUNT EZEKIEL IMEZUA BALAA!

Aunt Ezekiel akiwa na Mose Iyobo ‘Moze’.

SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa mjamzito, mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel imezua balaa baada ya mwanamke anayedaiwa kuibiwa bwana na mwigizaji huyo anayefahamika kwa jina la Mwengi kuibuka na kufunguka mazito.
Mwengi ambaye yupo ndani ya bifu zito na mwigizaji huyo, alizaa na dansa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo ‘Moze’ ambaye sasa inasemekana amekolezwa vilivyo na penzi la Aunt.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, siku chache zilizopita Mwengi alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo alitupia picha kibao zikimuonesha akilishana keki na Moze kuashiria kwamba wana mahaba niue huku akisindikiza na ujumbe huo wa kumtisha Aunt.
Mose Iyobo ‘Moze’ akiwa na familia yake.
“Kazi kwako shangazi hii ndiyo bethidei halali familia imetimia, toto langu la maana siyo wewe uliyetoa mimba kibao tutaona na hiyo mimba kama mtoto atazaliwa, haya mume wangu miye kazana kumchuna pesa huyo shangazi uniletee tutumie atakalia kuchunwa tu yeye shangazi kazi yake si kutoa,” aliandika Mwengi.
Mapaparazi wetu walipomtafuta Aunt ili kusikia anamzungumziaje Mwengi ambaye amemtupia madongo ya kutosha, simu yake iliita bila kupokelewa
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment