Mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyamisisi, Kata ya Kukirango, wilayani Butiama, Ryakora Kurwijira (34) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia shati lake akiwa ukweni baada ya kukataliwa na mkewe aliyekuwa akiishi naye.
Habari zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa karibu, zinaeleza kwamba
marehemu alikuwa akiishi na mkewe aitwaye Doy Nyanyara katika Kijiji cha
Nyatwari wilayani Bunda kwa kipindi cha miaka miwili, lakini ghafla
mwanamke huyo alimfukuza marehemu kutoka nyumbani na kumwambia kuwa
amepata mume mwingine wa kuishi naye, hivyo hamhitaji tena. Wawili hao
walikuwa wakiishi nyumba ya mwanamke.
“Baada ya marehemu kufukuzwa na mkewe aliondoka bila kuaga Jumamosi
iliyopita na kwenda nyumbani kwa wazazi wa mwanamke huyo huko Bariadi,
Simiyu na kujinyonga kwenye mti pembeni ya nyumba ya baba mkwe wake.
“Alipokaguliwa baada ya polisi kufika alikutwa na ujumbe unaosema:
“Nimejinyonga kwa ajili ya kupenda,” kilisema chanzo hicho.
Imedaiwa kuwa baada ya mwanaume huyo kujinyonga, wazazi wa mwanamke huyo walitokomea kusikojulikana, ambapo mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Bariadi kabla ya mwanamke huyo kuwapigia simu ndugu wa marehemu na kuwaambia kuwa ndugu yao amejinyonga.

Ndugu hao walifuatilia mwili huo na kuukuta katika hospitali hiyo
na kuuchukua kwenda kwao Kiabakari ambako mazishi yalifanyika Desemba 19
mwaka huu.
Afisa mmoja wa polisi wa Bariadi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Afisa mmoja wa polisi wa Bariadi ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment