Sanaa
ya Kutongoza(Art of Seduction) ni sanaa yenye mambo mengi,lakini mara
nyingi ni sanaa ambayo inaconcentrate kwenye attention ambayo wanaume
wengi wanapenda na wanataka kuipata kutoka kwa wanawake.
Leo nikaona si vibaya kama nikishare tips muhimu ambazo zitawasaidia kumpata mwanamke yeyote yule unaetaka kuwa nae,
1. JITAMBULISHE VIZURI KISTAARABU (INTRODUCE YOURSELF PROPERLY)
Kama
ndio umekutana nae kwa mara ya kwanza,hakujui na wewe humjui,ni vizuri
ukajitambulisha vizuri kwa ustaarabu(usela,mapozi na uhuni weka
pembeni),kama alikuwa anatembea unataka kumsimamisha,tumia lugha nzuri
kumsimamisha,na usije ukasimama ukadhani atakufuata,changamka mfuate
wewe,mkiwa mnatembea wote,jitambulishe vizuri,epuka maneno
yatakayomkera,usimuulize maswali yatakayochokonoa maisha yake binafsi
kwa kuwa bado hamjazoeana sana(Dont ask her personal questions)
2. ONGEZA MVUTO WAKO WA KIMWILI (UPGRADE YOUR PHYSICAL ATTRACTION)
Wanawake
wengi wanapenda wanaume wenye mvuto,wanapenda wanaume wenye miili
iliyojengeka kiume kimazoezi(six pack na blah blah nyingne za ziada),kwa
hiyo ili iwe rahisi kwako wewe kumshawishi(kumseduce) mwanamke
unayempenda,ni vizuri ukahakikisha mvuto wako upo juu tena sana.Kama ni
mnene au una kitambi anza kufanya mazoezi upunguze mwili.
Kuwa
Msafi(kama vipi oga hata mara 3 kwa siku),vaa vizuri upendeze,kwa
sababu first impressions zinalast longer kuliko unavyoweza kudhania.
3. WASILIANA NAE MARA KWA MARA (CONTACT HER FREQUENTLY)
Kila
mwanamke anapenda mwanaume ambaye atakuwa anamjali,Mwanaume atakaekuwa
teyari kusikiliza stori,matatizo na shida zake na kumsaidia
kusolve,Mwanaume ambaye atamfanya ajisikie Special muda wote .Na kitendo
cha wewe kuwasiliana nae mara kwa mara kitaonyesha kuwa unamuwaza muda
wote,kitaonyesha kuwa unamjali n.k na pia kitasaidia kuwafanya mzoeane
kidogo kitu ambacho ni kizuri kwako ukitaka kumake a move
4. KUWA MUONGEAJI MCHESHI (BE TALKACTIVE WITH A GREAT SENSE OF HUMOR)
Hakuna
Mwanamke anaependa kuwa bored,wanawake wengi wanapenda kucheka na kuwa
na furaha muda wote,kwa kuwa bado hajakuzoea sana,itabidi wewe ndio uwe
unaongea zaidi,jaribu kuongea mada(topics) ambazo anapenda(utajua kuwa
anapenda kwa kuangalia the way anarespond),ukianzisha mada ambayo
hapendi ni heri uiache uanzishe nyingine usije ukamboa.Pia jaribu
kumtania ili atabasamu au acheke lakini usivuke mipaka(limits),utani
unaweza ukawa wa kawaida lakini itapendeza zaidi ukiwa wa kimahaba.
5. NUNUA ZAWADI ZA KIMAHABA KWA AJILI YAKE(BUY ROMANTIC GIFTS FOR HER)
Unapokuwa
unachagua zawadi,usikimbilie kununua zawadi zenye Gharama kubwa
sana,kwa mwanamke aliyetulia mwenye akili zake timamu,atapata hisia
mbaya kwamba unataka kununua Penzi lake.(atahisi kuwa unataka kuchezea
hisia zake kisha umkimbie).Itakuwa vizuri kama ukinunua zawadi ambazo
sio expensive sana lakini ziwe na ujumbe wenye maana kimahaba.Unaweza
kumnunulia Apple,Chocolate,hereni n.k(just try to be more creative,t
always work).
0 comments:
Post a Comment