Viongozi wa CCM wakiongoza Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM
MBUNGE wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.
Hoja
ya kumvua uanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha
Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini
Zanzibar.
“Ni
lazima tumfukuze uanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya
kukinusuru chama hiki,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya
chama hicho.
Amesema,
“Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu.
Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru
chama chetu.”
Ajenda
ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika
kinachoitwa, “Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka
huu.”
Lowassa
alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete.
Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au
kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.
Januari
mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa “onyo” kwa kile
kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”
Mtoa
taarifa anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati
Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu
zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.
Lowassa
anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na
kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake
wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.
Anasema,
kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa
na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili
kukusanya kile kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”
Kutokana
na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na
kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada hao sita.
Mtoa
taarifa anasema, baada ya kikao cha Kamati ya Maadili kumalizika,
kutawasilishwa kwa Rais Kikwete pendekezo la kumfukuza Lowassa kutoka
katika chama hicho.
Mkutano wa Kamati Ndogo ya Maadili, utakuwa chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
Hata
hivyo, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, kuna uwezekano mdogo
mno kwa Kikwete kuweza kusimamia mradi huo hadi mwisho.
“Pamoja
na mkakati huo kuendeshwa na viongozi wajuu wa CCM, lakini bado
uwezekano wa kuutekeleza unakuwa mgumu. Hii ni kutokana na mwenyekiti
Kikwete kuwa kigeugeu,” anaeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa chama
hicho.
0 comments:
Post a Comment