Staa wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ au ‘Jojo’ amemrushia maneno makali aliyewahi kuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa hana akili timamu kufuatia maneno aliyotoa kuwa enzi za uhusiano wao, eti mwanadada huyo alikuwa akichenga kumzalia mtoto.
Katika mahojiano maalum ya hivi
karibuni kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha Runinga ya GlobalTV Online, Diamond alitoa madai kuwa, amekuwa akihaha kupata
mtoto.
Alisema kwamba, katika harakati zake hizo, warembo ambao alishatoka
nao kimapenzi akiwemo Jokate walikuwa wakimchezea mchezo mchafu ili
wasimzalie kwa kuwa alikuwa akiwaambia anahitaji mtoto kwa udi na
uvumba.
Hata hivyo, madai hayo ya Diamond
yalizua mzozo mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku warembo hao
wakipigwa za uso hivyo kutafuta namna ya kujitetea.“Hao akina…(wanatajwa
warembo wa Diamond) watakuwa wana matatizo ya uzazi siyo bure.
“Ndiyo maana Dangote (Diamond) ameona bora aende kwa Zari (msanii wa
Uganda, Zarinah Hassan) ambaye tayari ana mwanga wa kuzaa (ana watoto
watatu),” ilisomeka sehemu ya maoni juu ya madai hayo ya Diamond kwenye
Mtandao wa Instagram.
Diamond alifunguka:
“Jokate na Wema (Sepetu) nilitamani sana wanizalie lakini walikuwa
wakichengachenga, mambo mengine ujue si ya kuzungumza lakini inauma.”
Kufuatia tuhuma hizo nzito
huku kukiwa na madai pia, kwamba Jokate aliwahi kupigwa mimba
‘akaipanchi’, mwanadada huyo alipotafutwa na mwandishi wetu kujibu
‘shitaka’ linalomkabili alianza kwa kumshangaa staa huyo wa Ngoma ya
Ntampata Wapi inayokimbiza kwa sasa.
Jokate alisema anamshangaa
Diamond kuyazungumza maneno hayo hadharani na inaonesha asivyokuwa na
akili timamu au ambayo haijakomaa.
“Diamond atuache, kila siku anatuzungumzia, hana akili timamu.
“Inadhihirisha kweli hana akili kwa kuwa mtu mwenye akili zake timamu
hawezi kwenda kwenye chombo cha habari na kueleza hayo aliyoyasema,”
alisema Jokate akionesha kukasirishwa na maneno ya Diamond.
Ukiacha Jokate na Wema
ambaye naye aliwekwa kwenye kapu moja la kuchenga kumzalia, hakutaka
kumjibu Diamond kwa kuwa hataki malumbano au makuu na mtu.
Pia jamaa huyo alimzungumzia
aliyekuwa mwandani wake mwingine, Penniel Mwingilwa ‘Penny’ kuwa yeye
alitoa mimba zake mbili kwa visingio tofauti.
Katika majibu yake, Penny alisema kuwa Diamond awe mkweli na aseme tatizo lake kwani anavyojua yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.
Chanzo: Global publisher.
Katika majibu yake, Penny alisema kuwa Diamond awe mkweli na aseme tatizo lake kwani anavyojua yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.
Chanzo: Global publisher.
0 comments:
Post a Comment