Rais Mugabe Ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika [AU | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

Rais Mugabe Ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika [AU



Rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe, ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika AU akichukua nafasi ya Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania.
  
Mugabe mwenye umri wa miaka 90 ameteuliwa kwa kauli moja na Wajumbe katika mkutano wa AU unaoendelea kwa sasa mjini Addis Ababa-Ethiopia.
 
Imeelezwa kuwa uteuzi wa Mugabe kuongoza muungano huo mkubwa ulio na wanachama zaidi ya arobaini, huenda ukaleta doa ndani ya AU, kwa kuwa Mugabe hana uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kukaa madarakani tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru mwaka 1980.

SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment