Sentensi 3 za Profesa Jay siku ikitokea kakutana na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete…! | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

Sentensi 3 za Profesa Jay siku ikitokea kakutana na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete…!

Prof-JayIkiwa imebaki miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika kwa Tanzania,staa wa muziki wa Bongo Fleva ambaye amedumu kwa zaidi ya miaka 15 mtu mzima Profesa Jay anayo ya kusema na Rais Jakaya Kikwete.
Profesa Jay kwenye Exclusive na Amplifaya ametoa sentensi 3 ambazo kama akikutana na Rais leo angemwambia,sentensi ya kwanza amesema kuwa angemwambia Rais awe na maamuzi magumu kwa sababu kama tunachukia Rushwa na ufisadi basi na yeye awe mkali,atumie madaraka aliyonayo kwa sababu anaamini ana uwezo wa kuirudisha Tanzania kwenye mstari.
Sentensi yake ya pili  amesema angemwambia asicheke na Nyani kwani ndio maana anaona tunavuna mabua na huku akimsifia kwa kumwambia mheshimiwa unafanya kazi yako vizuri lakini wanaokuangusha ni watu waliokuzunguka.
Sentensi ya tatu ya Profesa Jay kwenda kwa Rais Kikwete amesema angemwambia Rais awe mkali zaidi atumie nafasi yake kama Rais ili Rushwa na Ufisadi vimalizike ili tuweze kuona matunda ya Tanzania.
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment