Mfanyakazi wa nyumbani, Hatibu Adamu (20) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kike wa miaka sita.
Akitoa
hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Said
Mkasiwa alisema kuwa upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi watano na
kwamba mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa.
Awali,
Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto alidai mahakamani hapo kwamba
kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ubakaji nchini, mshitakiwa huyo
apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.
Kabla
ya hukumu hiyo, Adamu alidai kwamba anasumbuliwa na vidonda vya tumbo
hivyo aliomba apunguziwe adhabu. Hata hivyo mahakama hiyo haikusikiliza
maombi hayo.
Mshitakiwa
huyo ambaye ni mkazi wa Majohe, Dar es Salaam, alidaiwa kwamba tarehe
isiyofahamika Septemba, mwaka jana, maeneo ya Majohe Wilaya ya Ilala,
Adamu alimlawiti mtoto huyo mwenye miaka sita huku akijua kufanya hivyo
ni kosa kisheria.
0 comments:
Post a Comment