Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
STAA wa
sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi
wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na
kuonekana wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
Lulu
alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani
mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa
wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.
“Nilijaribu
kuweka mawigi pembeni na kujisukia tano kichwa changu kwa kweli
naonekana katoto kabisa hapo ndipo nilipogundua kuwa mawigi kwa kipindi
kingine siyo kabisa yanatuzeesha tu,” alisema Lulu.
0 comments:
Post a Comment