...Akiwasihi wamuachie baada ya kufumaniwa.
JAMAA anayedaiwa
kwamba ni mpambe mkubwa wa mmoja wa wagombea urais mwakani ambaye ni
fundi wa kufunga madishi, mkazi wa Magomeni-Makanya jijini Dar es
Salaam, almaarufu Mgosingwa, amejikuta akivishwa shanga baada ya kunaswa
na mke wa mtu chumbani kwake.
Mgosingwa akivishwa shanga baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.
FUMANIZI
Tukio
hilo la aina yake la kufungia mwaka 2014 lilijiri kwenye fumanizi la
jamaa huyo lililochukua nafasi nyumbani kwake maeneo ya
Magomeni-Makanya, Dar, Jumanne iliyopita ambapo alifumwa na mke wa jamaa
aliyejitambulisha kwa jina moja la Faki aitwaye Mwanahamisi akidaiwa
kumrubuni kwa nguo za Sikukuu ya Krismasi.
Kwa
mujibu wa mwenye mke, baada ya Mgosingwa ambaye mkewe alikuwa safarini,
kunaswa laivu alitaka kuchoropoka kupitia dirishani lakini jamaa
alimkamata miguu na kumrudisha ndani.
Tulipofika
walikuta mtiti umeshika kasi ambapo kabla ya kufikia hatua ya
kudhuriana, polisi waliokuwa doria mtaani waliitwa na wasamaria wema na
kwenda kuokoa jahazi.
AVISHWA SHANGA
Polisi
walipofika walimkuta mwenye mke akiwa na shanga mkononi akimvalisha
Mgosingwa ambaye tayari hakuwa na ujanja.Hata hivyo, polisi hao
walifanya kazi ya ziada kumdhibiti mwenye mke ambaye alikuwa akipambana
nao akitaka aachiwe apambane na mgoni baada ya kumvisha shanga.
MAYOWE
“Niacheni jamani lazima na mimi leo nim….(tusi), haiwekani kabisa mtu atake kumdhalilisha mke wangu.
“Mke wangu nitajua cha kumfanya tukifika nyumbani, yaani ukweli nampenda sana mke wangu,” alisikika mwenye mke akipiga mayowe.
WAAMRISHWA WAVAE NGUO
Tukio
hilo lilisababisha mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo aliyejitambulisha
kwa jina la Mama Vicky na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Makanya (hakutaja
jina) wafike eneo hilo na kuwaamrisha waliofumaniwa wavae nguo kwanza.
SERIKALI YA MTAA
Baada
ya kuvaa, wahusika wote walipelekwa kwenye ofisi ya mtendaji wa mtaa
huo ili wazungumze na ikiwezekana wayamalize kwani wahusika hao walikuwa
‘hawajaduu’ bado.
January Makamba.
MSAMAHA
Baada
ya kufika ofisi ya mtendaji, Mgosingwa alimpigia magoti mwenye mke na
kumuomba msamaha huku akikiri kuwa alikuwa akitaka kula tunda la mkewe
lakini alikuwa bado hajathubutu kufanya hivyo hata siku moja.
“Chondechonde
kaka, mimi ni mwanaume mwenzako na wote, mimi, wewe na mkeo tunatoka
pamoja pale Makorora (Tanga) na familia zetu zinajuana fika.“Naomba
unisamehe ndugu yangu niko tayari kukulipa fidia ya kunishika ugoni,”
aliomba Mgosingwa.
Mgosingwa
aliendelea kuomba radhi ambapo mjumbe wa nyumba kumi na afisa mtendaji
walimshauri mwenye mke kupunguza jazba kisha akubali kuzungumza na mgoni
wake, wasifike mbali na kuyamaliza ili kuepusha usumbufu.
Benard Membe.
FAINI MIL. 1.5
Baada
ya kushauriwa kwa muda mrefu, mwenye mke aliiheshimu mamlaka hiyo ya
serikali na kukubali kulipwa faini shilingi milioni moja na nusu za
Kitanzania ili kumsamehe mgoni na kumpa onyo kali endapo wataendeleza
kamchezo hako.Baada ya hapo, Mgosingwa aliendelea kuwapigia simu ndugu
zake wamtumie fedha kwenye simu ili amalize tatizo hilo.
NI MPAMBE WA MGOMBEA GANI?
Kwa
mujibu wa majirani wa Mgosingwa ni mpambe wa mmoja wa wanasiasa maarufu
anayedaiwa kuwa kwenye ‘resi’ za kugombea urais mwakani, kufumaniwa
kwake kumetajwa pia kama ni njia mojawapo ya kumchafua mgombea
huyo.Mgosingwa alipoulizwa kama ni mpambe wa mgombea gani hakuwa tayari
kutaja.
WANAOTAJWA URAIS 2015
Baadhi
ya vigogo wanaotajwa kutaka kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015
ambao wana wapambe kila kona Bongo ni pamoja na Mizengo Pinda, Benard
Membe, January Makamba, Frederick Sumaye, Dk. Khamis Kigwangala, Dk.
Wilbrod Slaa, Wiliam Ngeleja, Steven Wasira, Dk. Mohamed Shein, Dk.
Emmanuel Nchimbi, Dk. Asha-Rose Migiro na Edward Lowassa.
0 comments:
Post a Comment