Frank Kalamu akiombewa kanisani.
MAAJABU! Ndivyo
unavyoweza kusema unapokutana na mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa
jina la Frank Kalamu (53) mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam, aliyetoa
ushuhuda wa kufunga mwaka kwamba kwa zaidi ya miaka miwili, alikuwa
akipata siku zake kama ilivyo kwa wanawake, ingawa yeye ni kupitia njia
ya haja kubwa.
Akitoa
ushuhuda huo ndani ya Kanisa (JINA KAPUNI) Desemba 21 mwaka huu, Frank
alidai amepata mateso hayo kwa muda mrefu huku akizunguka kwa waganga na
madaktari wengi bila mafanikio, mbaya zaidi, kwa kipindi chote hicho
ameshindwa kushiriki tendo la ndoa na mkewe.
Akizungumza
na paparazi nje ya kanisa, Frank alisema awali alikuwa mzima lakini
ghafla alianza kwa kukosa hamu ya kushiriki tendo na mkewe, ingawa
alipojaribu kuchepuka, alimudu vyema kazi hiyo.
“Baadaye dalili zilizidi kuongezeka, nikajikuta nikipata maumivu chini ya kitovu na kuanza kutoka damu kila mwezi hasa nikiwa najisaidia haja kubwa, hali hiyo huambatana na kutoka nyama sehemu za haja kubwa.
“Baadaye dalili zilizidi kuongezeka, nikajikuta nikipata maumivu chini ya kitovu na kuanza kutoka damu kila mwezi hasa nikiwa najisaidia haja kubwa, hali hiyo huambatana na kutoka nyama sehemu za haja kubwa.
“Nikawa
nikijisaidia kitu kama utumbo unatoka, huku damu zikitoka pia, siku
nyingine japokuwa ‘sikubleed’ lakini nyama hiyo ilitoka na nikawa
nairudishia kwa ndani,” alisema Frank kwa uchungu na kuongeza kuwa
alianza kuhangaika kwa waganga mbalimbali bila msaada wowote.
Baada
ya kuona anamaliza fedha bila kupata nafuu, Frank aliamua kutafuta
huduma ya kiroho ambapo akiwa kanisani hapo, Nabii Yaspi alimwambia kuwa
alikuwa amerogwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Saidi, ambaye mgonjwa
huyo alimtambua kama rafiki yake wa zamani aliyewahi kumhisi kuwa
alitembea na mchumba wake.
“Nabii
aliponiambia kuwa ni Saidi aliyeniroga, picha ya rafiki yangu ilikuja
kichwani, kila mara alinihisi natembea na mchumba wake. Nadhani
aliniroga kwa sababu hiyo si nyingine,” alisema mtu huyo ambaye pia
alidai kufuatia huduma ya maombezi anayoipata, anaanza kuona dalili za
mabadiliko ya hali yake.
0 comments:
Post a Comment