Rais wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha UDOM Masatu
Kyabwene amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu Dodoma kujihusisha na biashara ya
ukahaba kutokana na kukosa mikopo. Akizungumza na paparazi
alisema
“Kuna baadhi ya wanafunzi chuoni kwangu wana maisha magumu
sana kutokana na kukosa mkopo,wakati mwingine wananifuata
mimi na kunielezea shida zao ili niwasaidie,wengine ni yatima
hawana baba wala mama wa kuwalipia ada,siyo siri maisha ya
wanafunzi hawa ni magumu sana”
Tatizo la kucheleweshwa kwa mikopo limekuwa sugu sana katika
vyuo vikuu hapa tanzania ikiwemo chuo cha mzumbe morogoro
ambapo wanafunzi wa mwaka wa pili hawajui hatma yao ya
kupata mkopo tangu wapate matokeo yao ya mitihani.
Nini maoni yako kuhusu jambo hili?
0 comments:
Post a Comment