Jeshi
la polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road
wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki
katika jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni
tofauti kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa
ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA
BULIMBA ambaye mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo
haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na
vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga amani ya nchi na kwamba endapo
polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada
ya kumzika mwenzao aliyeuwawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa
mbaya zadi.
Kufuatia
tukio hilo paparazi imezunguka maeneo mbalimbali ya jiji yaliyodaiwa
kukumbwa na tafrani hiyo ambapo baadhi ya wananchi wa maeneo ya magomeni
ambako vurugu zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi kusababisha
watu kuanza kukimbia hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi na taarifa
kusambaa maeneo mengine.
Katika
maeneo ya mwananyamala na ubungo baadhi ya waliozungumzia sakata hilo
wameitaka serikali kuangalia makundi ya vijana na ikiwezekana wapatiwe
elimu ya ujasiriamali bure ili waweze kuendesha maisha huku wengine
wakishauri vijana wasiokuwa na kazi mitaani wapelekwe jeshini
wakafundishwe stadi za kazi pamoja na uzalendo ili kuepuka vitendo
hivyo.
Taharuki
hiyo ilitokea usiku wa tarehe mbili chanzo kikiwa ni kijana mmoja
aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuwawa na wananchi tarehe mosi
mwaka huu katika maeneo ya tandale kwa mtogole kwa tuhuma za wizi ambapo
tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia jeshi la polisi
zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga kufanya fujo ili
kulipiza kisasi.
0 comments:
Post a Comment