Panya Road" waliotiwa mbaroni wafikia 953 | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

Panya Road" waliotiwa mbaroni wafikia 953


Vijana 953 wanaodaiwa kujihusisha na vitenda vya kihalifu chini ya kundi maarufu la ‘Panya Road’ wamekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao wamekatwa katika mikoa ya kipolisi ya  Temeke na Ilala ambapo jeshi la polisi limefanya msako mkali kuweza kuwabaini.

Kamanda wa polisi Ilala, Mary Nzuki, alisema operesheni hiyo imefanyika kwenye  maeneo mbalimbali ya mkoa wao ikiwamo kwenye makutano ya wahuni wanaojihusisha na uvutaji bangi, dawa za kulevya na unywaji wa gongo.

Alisema operesheni hiyo iliyofanyika katika mikoa ya kipolisi, Temeke na Ilala,  imefikia idadi ya watuhumiwa hao  953 kutoka 624 ya juzi.

Alisema oparesheni hiyo ni endelevu na jeshi lake litaendelea kuwakamata vijana wote wanaozurura.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya Kihenya, alisema uchunguzi wa baadhi ya wahalifu waliokamatwa umekamilika na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Kihenya alisema 68 kati ya waliokamatwa katika mkoa wake ambao idadi yao ni 168 uchunguzi umekamilika na wamefikishwa mahakamani.
 
“Wapo wengine tuliwakamata kwa bahati mbaya, tumewaachia na 68 uchunguzi wao umekamilika, tumewafikisha mahakamani na wengine 100 uchunguzi dhidi yao unaendelea,” alisema.

Wakati huo huo, mtuhumiwa wa kikundi hicho aliyelazwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI)  aliyetambukika kwa jina na hali yake ya afya bado mbaya.

Meneja Uhusiano Moi, Jumaa Almasi, alisema mtuhumiwa huyo aliumia kichwani na kuvunjika mguu na amefanyiwa upasuaji wa mguu.
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment