Wema
Sepetu amekanusha kurudiana na mpenzi wake wa zamani Chaz Baba japo
amedai kuwa muimbaji huyo wa muziki wa dansi ndiye mwanaume wa pekee
ambaye hakuwa na masuala ya kiswazi baada ya kuachana.
Wema ameiambia U Heard ya Clouds FM Jumatano hii kuwa Chaz Baba kwa sasa ni mshkaji wake na hata alipooa alimchangia pesa.
“Chaz
Baba alikuwa ni msikaji wangu naweza kusema ndio boyfriend pekee asiye
na mambo ya Kiswahili,” amesema. “Tulizinguana tukafika pointi
tukasaidiana, ameoa nikamtolea mchango, nimeenda kwenye harusi yake
sioni tatizo.”
“Mimi
na Chaz Baba tulikuwa tunapendana na baada ya kufikia point ya kuachana
tukaachana, tukawa hatuongei for sometime mwisho wa siku baada ya kila
mmoja kukaa kwake tukawa tunazungumza. Sio kama watu wengine
tukigombanaga tunatafuta mabifu, hatusemeshani,” ameongeza mrembo huyo
aliyesisitiza kuwa ‘sina bwana’.
0 comments:
Post a Comment