VISABABISHI
Sasa wataalamu bado hawajawa na majibu kamili kuhusiana na tatizo hili la kutokwa na kijinyama katika maeneo ya haja kubwa husababishwa na kitu gani hasa lakini wameweza kutoa baadhi ya vitu ambavyo vinaaminika kwa kiwango kikubwa sana husababisha hali hii kujitokeza kwa mwanadamu, na vitu hivyo basi ni kama vifuatayo;

Kupata choo kigumu kupita kiasi kwa
mwanadamu wataalamu wanaita constipation mara nyingi imekuwa ni chanzo
kikubwa sana cha tatizo hili la mtu kutokwa na kinyama katika maeneo ya
haja kubwa na kuna uwezekano ikawa ni bawasili ya ndani au ya nje yenye
kuonekana, kwa hiyo kama mtu anakumbwa na hali ya kupata choo kigumu
basi kunauwezekano mkubwa sana mtu huyo akasumbuliwa na tatizo hili la
bawasili.
Hali ya kuharisha sana {heavy diarrhea},
kwa mtu ambaye anapatwa na hali ya kuharisha kwa muda mrefu basi naye
pia anauwezekano mkubwa sana wa kukumbwa na tatizo hili la kutokwa na
kijinyama katika maeneo ya haja kubwa au bawasili {hemorrhoid}.
Kukosekana kwa baadhi ya vyakula, kuna
baadhi ya vyakula vinapokosekana katika mwili wa mwanadamu au
visipotumika sana kwa mtu huweza kusababisha mtu kupata choo
kigumu kupita kiasi na kama anapatwa na hali hii basi kunauwezekano mkubwa sana mtu huyo akakumbwa na tatizo la bawasili na vyakula hivyo ni mboga za majani na matunda kwa wingi ndani ya mwili.
kigumu kupita kiasi na kama anapatwa na hali hii basi kunauwezekano mkubwa sana mtu huyo akakumbwa na tatizo la bawasili na vyakula hivyo ni mboga za majani na matunda kwa wingi ndani ya mwili.
Hali ya ujauzito kwa akina mama, hii pia
imekuwa ni sababu kubwa sana inayosababisha suala zima la kutokwa na
kijinyama maeneo ya haja kubwa na hii ni kwa sababu hali ya ujauzito kwa
mama husababisha kukua au kuongezeka kwa mji wa mimba ambao hutumika
hasa kumuhifadhi mtoto na kwa sababu hii basi inaweza kusababisha
vascular structure au vijinyama katika maeneo ya haja kubwa kwa mama
kuongezeka ukubwa na hivyo basi kuwa ni tatizo,
lakini mara nyingi mwanamke
akishajifungua kunauwezekano kikapotea lakini kama kinabaki basi ni vema
kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu zaidi.Kukaa kwa muda
mrefu, hali ya kukaa kwa muda mrefu kwa mwanadamu nayo pia imekuwa ni
kisababishi kikubwa sana cha tatizo kubwa la tumbo kujaa gesi na kupata
choo kigumu kupita kiasi {constipation}.
Mara nyingi watu wanaokumbwa na shida
hii kunauwezekano mkubwa sana wa kutokwa na kinyama au bawasili, hasa
kwa wanaotumia sana vyoo vya kukaa na kufanya hivyo kwa muda mrefu.
Hali ya wanadamu kunyanyua vitu vizito kupita kiasi kwa mwanadamu na ikawa ni zoezi endelevu kwa muda basi hali hii inaweza sababisha mtu kupatwa na tatizo la kutokwa na kijinyama au bawasili.
Itaendelea wiki ijayo.

0 comments:
Post a Comment