Makala : Hashim Aziz na mitandao
Umaarufu
wa msanii wa muziki, mjasiriamali na mkali wa fasheni kutoka Uganda
anayeishi Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari’ unazidi kupaa kila
kukicha, habari ya mjini kwa sasa ikiwa ni
Mfanyabiashara mkubwa wa Kiganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Ivan Ssemwanga akipozi.
Wengi
wanamjua Zari kutokana na urembo wa kipekee aliojaliwa na mkwanja wa
kufa mtu, akiwa anamiliki ndinga za bei mbaya zikiwemo Ranger Rover
Sports 2014, BMW, Black Chrysler, Audi Q7, Silver Crysler 2008, Mercedes
Benz Convertible na nyingine kibao, zote zikiwa na ‘plate number’
inayosomeka jina lake la Zari.
Hata
hivyo, ni wachache wanaojua siri ya utajiri wa mwanadada huyo ambaye
kiasili baba yake ana mchanganyiko wa Burundi na Somalia wakati mama
yake ana mchanganyiko wa Mhindi na Mganda.
IVAN SSEMWANGA NDIYO KILA KITU
Kabla
ya kuanza ‘projekti’ na Diamond, Zari alikuwa ameolewa na
mfanyabiashara mkubwa wa Kiganda mwenye makazi yake nchini Afrika
Kusini, Ivan Ssemwanga ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea
wachache kutoka Uganda, akiwa anaingiza faida ya zaidi ya shilingi za
Uganda milioni 700 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 428 za Kibongo).
MALI ANAZOMILIKI IVAN
Achana
na magari ya kifahari ambayo hayana idadi, yote yakiwa na ‘plate
number’ yenye jina la Ivan, mchizi pia anamiliki Private Jet (ndege
binafsi). Pia anamiliki utitiri wa vyuo vya Brooklyn City College,
vikiwa na jumla ya ‘campus’ sita nchini Afrika Kusini katika Majiji ya
Durban, Pretoria na Johannesburg, kila moja ikiwa na wanachuo kati ya
800 hadi 2100.
Kozi
zinazofundishwa kwenye vyuo vyake ni Information Technology (IT),
Mining (uchimbaji wa madini) na Policing (Sera za biashara) ambazo
zinapendwa na wengi Afrika Kusini, hali inayofanya apate wanachuo kibao.
Pia
jamaa anamiliki bonge moja la mjengo lililopo Sir Apollo Kaggwa Road,
Kampala pamoja na nyumba nyingine za kifahari zilizotapakaa maeneo ya
Munyonyo, Bunga, Mutungo na Mukono nchini Uganda.
Pia
jamaa anamiliki nyumba nyingine iliyopo Waterkloof Glen jijini
Pretoria, Afrika Kusini na kuwa miongoni mwa Waganda wachache
wanaomiliki nyumba nchini humo. Pia ana utitiri wa supermarkets, maduka
ya vito vya thamani na maduka ya nguo (boutique) nchini Afrika Kusini.
KUFURU YA FEDHA
Hivi
karibuni, Timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes ilikuwa na mechi dhidi
ya Timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) ambapo jamaa alifanya kufuru
ya aina yake kwa kutoa shilingi milioni 10 za Uganda (zaidi ya shilingi
milioni 6 za Kibongo) kwa kila mchezaji na kuahidi kutoa shilingi
milioni 5 za Uganda (zaidi ya milioni 3) kwa kila atakayefunga bao.
Zarinah Hassan ‘Zari’, 'The Boss Lady' akipozi.
Kama
hiyo haitoshi, jamaa alikodi helikopta iliyombeba yeye na wapambe wake
10 aliosafiri nao kutoka Afrika Kusini na kuwalipia kila kitu kuelekea
kwenye Mji wa Namboole, Uganda kushuhudia mechi hiyo ambayo hata hivyo
Uganda haikushinda.
AMETOKEA WAPI?
Ivan
aliyezaliwa kwenye familia yenye uwezo wa kawaida, alisafiri kwenda
Afrika Kusini akitokea Uganda mwaka 2002 kwa msaada wa mpwa wake,
Kyeyune aliyekuwa akifanya biashara ya magari ya kifahari Bondeni.
Baada
ya kukaa naye kwa kipindi kifupi, Ivan naye alianza kujishughulisha na
biashara hiyo ambapo alifanikiwa kutusua kinoma. Maisha yake
yakabadilika, akaanza kuwekeza kwenye biashara nyingine nyingi mpaka
akawa bilionea. Vijana wengi wa Afrika Kusini wanamtambua kwa jina la
Shaba Wa Shaba 9 kutokana na uwezo wake wa kifedha.
ANAMPAJE JEURI YA FEDHA?
0 comments:
Post a Comment