WEMA SEPETU, BOB JUNIOR SIO SIRI TENA, WATUMIA DAKIKA 10 KUONYESHANA MAHABA | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

WEMA SEPETU, BOB JUNIOR SIO SIRI TENA, WATUMIA DAKIKA 10 KUONYESHANA MAHABA

LICHA ya Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwahi kufikishwa kortini na Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior, wamebambwa ‘live’ wakioneshana mahaba niue, Amani lina tukio zima.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa mapajani mwa Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior'.
TUJIUNGE TEGETA, DAR Ishu hiyo iliyopigwa chabo na paparazi wetu hivi karibuni lilijiri ndani ya Ukumbi wa Club 71 uliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo Wema siku hiyo alimtambulisha msanii wake mpya anayesimamiwa na kampuni yake ya Endless Fame anayeitwa Ally Luna.
WAKUTANA Katika tukio hilo, Wema ndiye aliyeanza kufika ukumbini humo akifuatana na timu yake, akiwemo Petit Man (kama kawa). Muda mfupi baadaye, Bob Junior naye alifika ambapo alipokutana na Wema walianza kupeana mahaba huku wakigandana kwa zaidi ya dakika kumi.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akizidi kupozi kimahaba na ‘Bob Junior'.
Mbali na Bob Junior, Wema alialika wasanii kibao kwa ajili ya kumsapoti ambao hata wao walipigwa butwaa baada ya kushuhudia tukio hilo. Wakiwa katika chumba cha VIP, Wema aliendelea kuwa ‘veri klozi’ na Bob Junior hivyo kusababisha minong’ono ya hapa na pale.
MAPOZI Katika tukio hilo, kilichowashangaza mashuhuda zaidi ni kitendo cha Wema kukaa mapajani kwa Mbongo Fleva huyo bila kujalia macho ya watu.
Wema Sepetu na ‘Bob Junior' wakiteta jambo.
SALAMU KWA DIAMOND NA ZARI? Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walikwenda mbali zaidi na kuanza kuhisi tabia hiyo ya Wema na Bob Junior ni salamu kwa aliyekuwa mwandani wake na kumwagana Nasibu Abdul ‘Diamond’ na ‘bebi’ wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Hapa naona kama sielewielewi maana ni mara ya kwanza kumwona Wema na Bob Junior wakigandana kiasi hiki tangu walipopelekana mahakamani kipindi kile na ukizingatia Sharobaro (Bob Junior) alikuwa hasimu wa Diamond aliyekuwa mpenzi wa Wema kipindi hicho,” alisema mmoja wa mastaa wakubwa (jina linahifadhiwa). Akaongeza:
Wema Sepetu akimchumu ‘Bob Junior.
“Nakuhakikishia hizi ni salamu kwa Diamond na yule Zari wake. Hapa Wema anajua kabisa salamu zitawafikia.” Baadhi ya mastaa hao walionekana kulaani tukio hilo na kujaribu kumtahadharisha Wema juu ya ukaribu huo kwani kama Diamond atagundua atajua ni ishu za kulipizana visasi. “Kwa vyovyote Diamond akigundua jambo hili litamfanya ukaribu wake na Wema kuzidi kuwa mgumu na kuurejesha ni ndoto kama wana mpango wa kurudiana.”
WENYEWE WANASEMAJE? Paparazi wetu alipojaribu kuwadodosa wawili hao juu ya uhusiano wao, kila mmoja aliishia kucheka tu bila kutoa majibu ya kueleweka.
DAKTARI AMUONYA WEMA
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment