Acha kabisa! Mazishi
ya baba wa mastaa wa muziki wa Nigeria, mapacha Peter na Paul Okoye
wanaounda ‘Kruu’ ya P-Square, Moses Okoye aliyefariki dunia Novemba 24,
2014 yamekuwa kama sherehe, Ijumaa Wikienda limedodosa kilichojiri.
Ishu hiyo ilijiri nyumbani kwa mastaa
hao eneo la Ifitedunu, Jimbo la Anambra nchini humo Ijumaa iliyopita
ikiwa ni siku 65 tangu mzee huyo alipofariki dunia baada ya kufanyiwa
oparesheni ya goti alipodondoka kwenye ngazi nyumbani kwake maeneo hayo.
Wakina P-square wakiwa na wake zao katika msiba huo.
Tofauti na ilivyozoeleka kwamba kwenye
msiba watu huwa wanalia na kuomboleza, mazishi hayo yaliyohudhuriwa na
mastaa kibao nchini humo yalikuwa tofauti kwani watu walikuwa na nyuso
za tabasamu huku wakiserebuka na matarumbeta juu.
Ulinzi mkali ukiimarishwa katika msiba huo.
Mbali na kuonekana kuwa kama sherehe,
pia mazishi hayo yaliripotiwa kuwa ya gharama zaidi kuanzia jeneza
lililobeba mwili wa baba yao, gari ‘spesho’ lililokuwa na jina la Dady
badala ya namba za usajili na wahudhuriaji waliopiga sare nyeupe huku
wakijifotoa picha wakicheka na kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Mwili wa baba wa P-Square ukiwa kwenye jeneza
Pia kivutio kikubwa kilikuwa ni wake wa
mastaa hao ambao walipewa ulinzi mkali uliowekwa katika mazishi hayo
yaliyohudhuriwa kwa mualiko maalum.
Baba wa P-Square (aliyenyosha mikono) enzi za uhai wake.
Cha kushangaza, wakati mwili wa baba yao
ukiwa mochwari, jamaa hao walidaiwa kuendelea na ratiba za kimuziki
huku wakifanya shoo kama kawa jambo ambalo kwa Bongo haliwezekani.Kwa sasa mastaa hao hawana mzazi hata mmoja baada ya mama yao naye kufariki dunia mwaka 2012
0 comments:
Post a Comment