KESI YA MAUAJI YA BILIONEA MSUYA YAIVA | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

KESI YA MAUAJI YA BILIONEA MSUYA YAIVA


Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, imesema taratibu zote kwa ajili ya kuanza usikilizaji wa kesi ya mauaji ya kukusudia dhidi ya bilionea wa madini ya Tanzanite, mkoani Arusha, Erasto Msuya (pichani), inayowakabili wafanyabiashara na wachimbaji saba wa madini hayo, zimekamilika.
 Kwa mujibu wa barua ya Msajili wa Wilaya na Mahakama Kuu ya Tanzania, iliyoandikwa na kusainiwa na H.S. Mushi, Januari 26, mwaka huu, kesi hiyo namba 06 ya mwaka 2013, itaanza kunguruma mjini hapa, Februari 10, mwaka huu.
Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi 13, Agosti 07 mwaka 2013, saa 6:30 mchana, kando ya barabara kuu ya Arusha-Moshi, eneo la Mijohoroni, Wilaya ya Hai, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na kufariki papo hapo.
Sehemu ya barua hiyo, paparazi imeona nakala yake, inaeleza kwamba Mahakama Kuu, itaanza usikilizaji wa awali wa kesi za mauaji Februari 4 hadi 10, mwaka huu, baada ya kukamilisha maandalizi ya vikao vya kesi za mauaji katika Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi na Kituo cha Rombo, kati ya Februari na Mach
Wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Sharif Athuman (31), mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha; Shaibu Saidi maarufu kama Mredii (38), mkazi wa Songambele Wilaya ya Simanjiro na Mussa Mangu, (30), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu mkoani Arusha.
Wengine ni Jalila Said (28), mkazi wa Babati, Sadiki Jabir a.k.a “Mnubi”(32), mkazi wa Dar es Salaam na Lang’ata wilayani Hai; Karim Kihundwa (33), mkazi wa Kijiji cha Lawate, Wilaya ya Siha na Ali Majeshi, mkazi wa Babati, mkoani Manyara.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa la mauaji ya kukusudia, kinyume cha kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment