Mvutano
mkubwa umeibuka kati ya Jeshi la Polisi na vijana waliopata mafunzo ya
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kufuatia kupotea kwa Mwenyekiti wao wa
Vijana, George Mgoba, katika mazingira ya utatanishi.
Hata
hivyo, viongozi wa vijana hao wamehojiwa kwa zaidi ya saa nane katika
kituo cha polisi kati kwa kile polisi walichokiita walikuwa wakizungumza
nao kuhusu madai yao.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Askari hao, Parali
Kiwango, alisema mwenyekiti wao alipotea Jumatatu, majira ya saa ya saa
3:00 nyumbani kwake Mabibo Royola. Alisema tangu siku atoweke, hawana
mawasiliano naye baada ya namba za simu zake za mikononi kuwa zimezimwa.
Kiwango
alisema kwa mujibu wa mke wake, Mgoba alipigiwa simu na mtu ambaye
hajafahamika akimtaka wakutane eneeo la Mabibo mwisho, alipoondoka
hakurejea tena.
“Kwa
mujibu wa mke wake anasema mtu huyo alijitambulisha kwa askari
mwenzake, lakini sisi hatukumpigia simu ya aina hiyo, tunajua vyombo vya
usalama vimehusika,” alisema Kiwango
Vijana
hao waliomaliza mafunzo yao ya kijeshi katika kambi mbalimbali za JKT
nchini, wamekuwa wakidai kupewa ajira kulingana na mafunzo waliyopewa.
Hata
hivyo, wametishia kuitisha maandamano ya siku tatu yatakayoishia Ikulu
ili kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kusikiliza kilio chao.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akizungumza
ofisini kwake, alikana jeshi hilo kuhusika na kupotea kwa Mgoba na
aliahidi kutoa kauli kuhusu suala muda utakapofika.
Viongozi wa vijana hao wamehojiwa na polisi kwa muda wa saa tisa kwa kile kinachoelezwa kuzima jaribio la mandamano.
Akizungumza
mara baada ya kikao hicho, Kiwango alisema walihojiwa na maafisa wa
ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuhusu madai
ya wao kutaka kuandamana.
Alisema
mahojiano hayo yalianza kufanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi majira
ya saa 7:00 mchana na kupewa mapumziko mafupi na illipofika saa 8:00
waliitwa Ofisi ya Kova na kuhojiwa hadi saa 10 jioni walipoachiwa.
0 comments:
Post a Comment