Hukumu
hiyo ilikuja baada mshitakiwa huyo kupinga kifungo cha miaka 15
alichopewa na Mahakama Kuu Zanzibar baada ya upande wa mashtaka kupinga
uamuzi wa mahakama ya Mkoa wa Vuga, kumuachia huru mshitakiwa.
Adhabu hiyo ilitolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar,Abdul- hakim Ameir Issa.
Uamuzi
wa kumuachia huru mshitakiwa huyo katika mahakama ya Vuga, ulitolewa na
Hakimu Makame Mshamba Simgeni, baada ya kusema ushahidi uliotolewa na
upande wa mashtaka hautoshi kumtia hatiani.
Jopo
la majaji watatu akiwemo Jaji Kimano, Jaji Njasiri na Jaji Luonda,
walitupilia mbali rufaa ya mshitakiwa kupinga kifungo hicho na badala
yake ikaamua kumuongezea kifungo cha miaka 15.
Adhabu hiyo mpya sasa inamfanya mshitakiwa huyu kutumikia kiufungo cha miaka 30 jela.
Wakitoa
hukumu, majaji hao walisema vitendo hivyo vimekithiri licha ya kukemewa
na Serikali na kwamba adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa wengine wenye
tabia kama hiyo.
Hukumu
hiyo ilitolewa Februari 13 mwaka huu huku upande wa mashtaka
ukiwakilishwa na Maulid Ame Mohammed kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka.
0 comments:
Post a Comment