Baadhi
ya watu wakiangalia moja ya nyumba za mganga wa kienyeji
zilizoteketezwa kwa moto na wananchi wa vitongoji vya Kazunzu, kijiji
cha Nyambemba, kata ya Kazunzu na wa kitongoji cha Lueseselo
Wananchi
wa vitongoji vya Kazunzu, kijiji cha Nyambemba, kata ya Kazunzu,
wakishirikiana na wa kitongoji cha Lueseselo, kata ya Bulyaheke,
wamempiga kwa marungu, mawe na mapanga na kisha kumchoma moto mtu
ambaye bado hajafahamika, wakimtuhumu kuwa wakala wa kuteka watoto
wakiwamo walemavu wa ngozi (albino), akishirikiana na waganga wa
kienyeji wapiga ramli kwa imani za kishirikina za kupata utajiri.
Mbali
ya kumuua, wananchi hao pia wamevunja na kuchoma moto nyumba 13
zilizoezekwa kwa bati mali ya mganga wa kienyeji mwanamke mpiga ramli
mwenye umri wa miaka 40 (jina linahifadhiwa).
Hata hivyo, mganga huyo na familia yake walifanikiwa kuwatoroka wananchi hao.
Tukio
hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata
Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha
Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Richard
Mangalamu baba wa mwanafunzi aliyetekwa, Winfrida (11) anayesoma darasa
la nne Shule ya Msingi Kazunzu, alisema mtuhumiwa alimwachia mwanafunzi
huyo kutokana na kumkuta ana chale mgongoni na kifuani akidai amepoteza
ubora.
Mkuu
wa Polisi wa Kituo cha Wilaya ya Sengerema, Babu Sanare na Ofisa
Mtendaji wa kata hiyo, Enock Mabula, kwa nyakati tofauti walithibitisha
kutokea kwa tukio hilo.
Naye
Diwani wa Bulyaheke, Bagadi Nyuki, akiwa eneo la tukio, alisema chanzo
cha mauaji hayo ni marehemu kudaiwa kuwa juzi alimteka mwanafunzi wa
kike anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Kazunzu na kumvutia
vichakani na kisha kumvua nguo na kumpapasa.
Inadaiwa
kuwa alimuachia huru baada ya kugundua kuwa hakuwa na sifa
zinazohitajika na mganga na mwanafunzi huyo alipofika nyumbani
aliwaeleza wazazi wake na ndipo wakishirikiana na wanakijiji wenzao
walianza kumsaka mtuhumiwa na kufanikiwa kumtambua.
Inadaiwa
baada ya kubanwa mtuhumiwa huyo alikiri na kujitambulisha alikuwa
ametoka kijiji cha Katoro, mkoani Geita na alikwenda Sengerema kwa kazi
ya uwakala wa kuteka watoto.
Diwani
huyo alisema marehemu aliomba apelekwe kijiji jirani cha Bulyaheke
umbali wa kilometa sita kutoka Kazunzu kwa mwenyeji wake na mdau
mwenzake, Sato, lakini wapofika walikuta amekwisha kutoroka.
0 comments:
Post a Comment