"Ni ajali ambayo haijawahi kutokea katika maeneo haya," ni
baadhi ya maneno yaliyosikika kutoka kwa wakazi wengi wa mjini Mafinga
na vitongoji vyake, ambao jana walishuhudia ajali katika historia ya
mji huo.
Ajali
hiyo ilihusisha lori aina ya Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex
Company lililokuwa likiendeshwa na Maka Sebastian (26) na basi aina ya
Scania namba T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa
likiendeshwa na Baraka Gabriel (38).
Wakati lori lilikuwa likielekea Barabara ya Mafinga-Mbeya, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
Ajali
hiyo iliyosababisha vifo vya watu 42 wakiwemo 40 waliokuwemo katika
basi na wawili katika lori hilo, ilitokea katika eneo la Changarawe
takribani kilometa 5 kutoka mjini Mafinga, mkoani Iringa, katika
barabara kuu ya Mafinga-Mbeya.
Kati
ya waliokufa yupo dereva wa basi hilo, huku dereva wa lori akijeruhiwa
vibaya baada ya kuchomwa na kitu kama nondo shingoni mwake.
Akiwa
ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mwenyekiti wa
Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Asas na baadhi ya
wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, Mungi alisema ajali hiyo
ilitokea jana asubuhi saa tatu na nusu.
Kamanda
Mungi alisema jeshi lake kwa kushirikiana na hospitali za Mafinga na
Mkoa wa Iringa wanaendelea kutambua majina ya watu waliokufa na
majeruhi.
Kamanda
Mungi alisema taarifa zao za awali zinaonesha chanzo cha ajali hiyo ni
ubovu wa barabara. Mungi alisema lori na basi hilo yaligongana uso kwa
uso wakati madereva wake wakishindana kuwahi kuchepuka moja kati ya
mashimo makubwa yaliyopo pembezoni na katikati mwa barabara hiyo katika
eneo hilo.
Baadhi
ya watu waliotajwa kuwepo katika basi na lori hilo ambao hata hivyo
hawakuweza kufahamika mara moja, nani kafa na nani kajeruhiwa ni pamoja
na Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni na
Frank Chiwango.
Wengine ni Luteni
Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine,
Mbamba Ipyana, Catherine, Mwajengo, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala,
Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin
Haule na Dominick Mashauri.
Wengine ni Ester
Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula,
Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto
Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge na Juma Sindu.
Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.
Habari
kutoka Mbeya zinaeleza kuwa wakati basi hilo linaondoka kituoni abiria
waliokuwepo kwenye basi hilo walikuwa ni 37 ambao ni:
Baraka
Ndone ambaye ni dereva, Yahya Hassan ambaye ni kondakta, Esther
Emmanuel, Henry Lugano, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Hamad, Olga
Solomon, Neto, Theresia Kaminyoge, Frank Chiwanga, Luteni Sanga, Alfred
Sanga, Doto Katunga, Juliana Bukuku, Esther Fidel, Paulina Josia.
Wengine ni Iman
Mahenge, Catherine Mwate, Mathias Justine, Rebeka Kasambala, Upendo
William, Mbamba Ipyana, Ndulile Kasambala, Dk A. Shitindi, Six Erick,
Frank Mbaule, Mustafa Ramadhani, Musa, Omega Mwakasege, Shadra Msigwa,
Lucy Mtanga, Charles Mweisonga, Martin Haule, Dominick Mashauri, Kelvin
Ebadi, Juma Saidi, na Nicko
0 comments:
Post a Comment