Kwenye nafasi nyingi za kazi siku hisi tunakutana na vitu na mambo mengi. Kazi nyingi zinatangazwa kisiasa lakini zinakuwa na watu tayari. Lakini hapa nataka kuzungumzia kazi ambazo bado hazina mikono ya watu sana.
Hivyo watu wengi huenda kwenye usaili wakihofu sana wenzao waliotangulia au watakaofuata watafanyaje, wasiwasi huo mara nyingine unaweza ukaathiri namna ambavyo utafanya usaili huo. Hutakiwa kuwa na wasiwasi wa vitu ambavyo huna uwezo navyo au hauna maamuzi navyo fanya yanayokuhusu na mambo mengine yataendelea. Fikiria kufanya vizuri kwenye usaili wako kwa kujua siri hii:
1. Zingatia Uwezo wako wa kipekee
Kila mtu anatakiwa kuwa na ujuzi fulani wa kipekee na huo ndio ujasiri utakaokuingiza kwenye usaili bila wasiwasi. Je uwezo wako binafsi katika ujuzi huo uko wapi, labda ni mzuri katika utafutaji wa masoko, au mauzo na onyesha mifano ya vitu ambavyo umeweza kuvifanya.
2. Toa mifano halisi inayojulikana
Watu wengi wana CV ambazo hazina vitu vya msingi ndani yake hivyo mwajiri anakuwa haoni kama ni mtu anayestahili nafasi fulani. Ili kuepusha hilo hakikisha CV yako imeshiba vitu halisi ambavyo umefanya hapo nyuma au kwenye kazi yako ya sasa. Hivyo vitu vinatakiwa kuwiana na kazi unayoomba!
3. Uwe na ushahidi unaobeba mifano yako katika maandishi
Mahesabu au majeduari yanaweza kuonyesha namna gani ujuzi wako unafanya kazi na una weredi wa kiasi gani. Je uliongeza mapato, uliweza kupunguza matumizi au uliokoa muda kwenye kazi liyopita? Je uliweza kupata wateja wangapi kwenye kazi iliyopita kwa mwaka? au Mauzo yako yalikuwaje kwenye kitengo chako?
4. Onyesha kwa vitendo ujuzi wako
Watu huajiri watu wanaowapenda. Wakati wa usaili unahitaji kuonyesha uwezo wako wa kuwasiliana vizuri. Je! unahusiana vipi na watu? Je wewe ni muadilifu na vinginevyo unavyohitaji kuonyesha!
5. Sahau ushindani, fanya yanayokuhusu
Ili kuondokana na ushindani usiokuwa na sababu achana na kuwa na wasiwasi na watu wengine. Huhitaji msongo wa mawazo mwingine wakati wa kutafuta kazi, ila fikiria utaleta mchango gani kwenye kampuni unayoiendea.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment