Waziri sitta kuwachukulia hatua waliofanya ufisadi katika uagizaji wa mabehewa mabovu TRL | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

Waziri sitta kuwachukulia hatua waliofanya ufisadi katika uagizaji wa mabehewa mabovu TRL


Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema kuwa mabehewa yaliyoingizwa nchini kutokea Kampuni ya M/S Hindusthan Engeneering Industries Limited yapo chini ya kiwango na hivyo wale ambao wamehusika na ukaguzi na kufanya mabehewa hayo yaingizwe nchini watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara alipotembelea Shirika la Reli Nchini (TRL),Sitta alisema serikali ikithibitisha waliokagua na kuleta mabehewa hayo watachukuliwa hatua.“Nchi hii ni masikini hivyo wote waliohusika katika uingizaji wa mabehewa hayo watachukuliwa hatua kutokana na sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kusitisha mkataba  huo na hili nitafuatutilia kwa karibu na bodi ya TRL nimeiagiza kufanya hivyo”alisema Sitta.
Alisema kutokana na kuingizwa kwa mabehewa yasio na ubora,wamezuia kuingia tena kwa mabehewa 124 kutokana na mkataba walioingia nao wa kuleta mabebewa hayo.
Sitta alisema hali ya shirika ni nzuri kutokana mapato yake kuongezeka kutokana na watendaji kujipanga katika uendeshaji wa shirika hilo.  
Waziri wa Uchukuzi,Mh. Samwel Sitta (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo,wakati alipotembelea Shirika la Reli nchini (TRL). kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mh. Charles Tizeba na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Monica Mwamunyange,.
Sehemu ya Wanahabari wakimsikiliza Waziri Sitta (hayupo pichani) wakati alipotembelea Shirika la Reli nchini (TRL) jijini Dar leo
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment