Vurugu kubwa zimezuka, yakachomwa
matairi ya magari barabarani.. hakuna basi lolote la abiria kwenda
mikoani lililokuwa limetoka wala hakuna daladala iliyokuwa ikipakia
abiria katika eneo hilo.
Baada ya kuanza vurugu Polisi waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya.
Muonekano wa stendi ya mabasi Ubungo kwa juu, hakuna gari hata moja ambayo ilisafiri kwenda Mikoani leo.
Barabarani hazionekani gari za abiria, watu wanatembea kwa miguu.
Wengine walizuia hata gari za watu binafsi kuonekana ikipakia abiria yoyote.
Baadi ya maeneo usafiri ni bodaboda, Noah na magari binafsi. Wengine wanatembea kwa miguu.
Askari Polisi wakitoa matairi wa magari yaliyowekwa Ubungo
Kuna baadhi ya watu waliokamatwa kwa kuhusika na vurugu hizo
Gari la Polisi likitoa matairi yaliyowekwa barabarani na kuchomwa moto.
Madereva hao wamegoma kutokana na sababu mbalimbali, mojawapo ni shu ya utaratibu wa kutakiwa kwenda Chuoni kusoma tena baada ya muda wa leseni zao kuisha
0 comments:
Post a Comment