BREAKING NEWS: MGOMO WA MADEREVA WAANZA ASUBUHI YA LEO SEHEMU MBALIMBALI NCHINI | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

BREAKING NEWS: MGOMO WA MADEREVA WAANZA ASUBUHI YA LEO SEHEMU MBALIMBALI NCHINI


Mgomo  wa  Madereva  umeanza  rasmi  leo  katika  maeneo  mbalimbali   nchini kama ambavyo muungano wa madereva wa vyombo vya usafiri waliahidi wakidai kutotatuliwa kero zao na serikali.
Sababu  kubwa  ya  madereva  hao  kugoma  ni  kuishinikiza  serikali  kuweka  mfumo  mzuri  wa  ajira  na  kupinga  kanuni  inayowataka  kurudia  kusoma  katika  chuo  cha  taifa  cha  usafirishaji,NIT  kila  leseni  zao  zinapokwisha  muda. 
Madereva  hao  wanadai  malalamiko  yao  makubwa  ni  kitendo  cha  Serikali  kuongeza  kifungu  kidogo  katika  sheria  mpya  ya  mwaka  2015  namba 31  inayowataka  madereva  wote  wenye  leseni  za  madaraja  E,C1,C2,C3  na  C kurudi  darasani  kila  baada  ya  miaka  mitatu  kuongeza  utaalamu  katika  fani  hiyo  ya  udereva  ili  kupunguza  ajali  za  mara  kwa  mara  zinazotokea. 
 
Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.

SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment