HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

Siwema wa Nay wa Mitego Yazidi Kumkuta..Apandishwa Kizimbani Kwa Kosa la Kujipatia Mali na Pesa Kwa Vitisho

MAJANGA yamezidi kumkuta mzazi mwenzake na Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson ambapo jana alitarajiwa kufikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, kujibu shitaka la kujipatia mali kwa njia vitisho.

Siwema anatuhumiwa kujipatia mali kwa kumtishia kigogo mmoja serikalini (jina tunalihifadhi) ambaye inadaiwa alikuwa mchumba wake na baada ya kuachana, mrembo huyo kwa nyakati tofauti akawa anamtishia kuwa ana picha zake za utupu hivyo asipompa fedha ataziweka mitandaoni hivyo kigogo huyo alikuwa akilazimika kumpatia.

Chanzo cha habari hii kimeeleza kwamba, baada  ya polisi kujiridhisha na uchunguzi wa madai hayo, waliamua kumpeleka mahakamani ili kujibu shitaka hilo linalomkabili.

“Kesho (jana) wanampandisha mahakamani akajibu shitaka linalomkabili maana polisi tayari wameshamaliza uchunguzi wao hivyo sakata hilo linahamia mahakamani,” kilisema chanzo chetu.

 Alipotafutwa Siwema kwa njia ya simu, simu yake iliita bila majibu lakini alipopigiwa msaidizi wake wa dukani aitwaye Zuhura, alisema:

“Dada (Siwema) jana alikuwa polisi hivyo sijajua kama wamempeleka mahakamani au la!”

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo alikiri kumkamata Siwema kwa kosa la kujipatia mali kwa njia ya vitisho kisha kumuachia kwa dhamana

Mashambulizi kwa wageni Afrika Kusini bado ni ishu kubwa, hii ni ripoti nyingine kutoka huko (VIDEO)

Xenophobia-In-South-Africa-Nigerians-Victims-650x398
Stori ya ishu ya ubaguzi Afrika ikarudishwa kwenye headlines na matukio ya South Africa.. Xenophobia ikachukua nafasi ya ripoti nyingi za habari kubwa Afrika kwa zaidi ya mwezi mmoja, kwa sasa hivi ni kama hali imetulia japo sio kwa asilimia 100 !!
Wenyeji wanahofu kuendelea kuwepo Afrika Kusini, hii imeripotiwa na kituo cha TV  cha SABC Afrika Kusini, wageni wengine 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliamua kuanza safari ya kurudi kwao ikiwemo Wamalawi.
Watu zaidi ya 100 walilazimika kurudi kwenye nchi zao kutokana na kuanza kwa vurugu za mashambulizi ya wenyeji wa South Africa waliokuwa wakiwafukuza wageni.. wengine waliuawa na wapo waliojeruhiwa na kupoteza mali zao pia kutokana na mashambulizi hayo.
Nataka nirudi nyumbani kwa sababu huku hali sio nzuri.. wanatupiga, wanataka kutuua nimeona nirudi tu nyumbani“– Hassan Shalifa, mmoja ya raia wa kigeni waliokuwa wakijiandaa kuondoka South Africa.

I'm Now Dating GK But I Would Love To Have a 2nd Child With Chris Brown: Diva Loveness Malinzi

Hot Radio presenter from Tanzania, Diva Loveness Malinzi wants to have a 2nd child with American superstar Chris Brown. Diva believes her child will be so cute if the father is Chris Brown. Through instagram the controversial presenter who is currently dating Bongofleva artist King Crazy GK shared video of Chris Brown's daughter and she had the below to write.....

What do you think considering Diva is currently in a relationship with GK.....?

Sentensi 3 za Profesa Jay siku ikitokea kakutana na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete…!

Sentensi 3 za Profesa Jay siku ikitokea kakutana na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete…!
Prof-JayIkiwa imebaki miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika kwa Tanzania,staa wa muziki wa Bongo Fleva ambaye amedumu kwa zaidi ya miaka 15 mtu mzima Profesa Jay anayo ya kusema na Rais Jakaya Kikwete.
Profesa Jay kwenye Exclusive na Amplifaya ametoa sentensi 3 ambazo kama akikutana na Rais leo angemwambia,sentensi ya kwanza amesema kuwa angemwambia Rais awe na maamuzi magumu kwa sababu kama tunachukia Rushwa na ufisadi basi na yeye awe mkali,atumie madaraka aliyonayo kwa sababu anaamini ana uwezo wa kuirudisha Tanzania kwenye mstari.
Sentensi yake ya pili  amesema angemwambia asicheke na Nyani kwani ndio maana anaona tunavuna mabua na huku akimsifia kwa kumwambia mheshimiwa unafanya kazi yako vizuri lakini wanaokuangusha ni watu waliokuzunguka.
Sentensi ya tatu ya Profesa Jay kwenda kwa Rais Kikwete amesema angemwambia Rais awe mkali zaidi atumie nafasi yake kama Rais ili Rushwa na Ufisadi vimalizike ili tuweze kuona matunda ya Tanzania.

Breaking News: Watu 10 Wafariki Dunia Baada ya Basi la kampuni ya Unique Kugongana na Gari la Coca Cola


Habari  zilizotufikia  zinaarifu  kuwa  basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.

Watu 10 wamefariki na  50 wamejeruhiwa.Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.






Bilionea Namba Moja Africa Dangote Akagua Ufukwe Atakao Jenga Bandari yake ya Kisasa Mtwara

Biionea Alhaji Aliko Dangote amekabidhiwa hekari 2,500, katika halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ili ajenge bandari itakayotumika kusafirisha saruji kutoka kiwandani hapo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.




Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo


Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa

KAMANDA MKUU WA BOKO HARAMU AUAWA, NGOME YAO YASAMBALATISHWA

KAMANDA MKUU WA BOKO HARAMU AUAWA, NGOME YAO YASAMBALATISHWA
Meja Jenerali Chris Olukolade.

Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa, vikosi vya nchi hiyo vimemuua kamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.

Meja Jenerali Chris Olukolade amesema kuwa, Abu Mojahid kamanda wa ngazi za juu wa kundi la Boko Haram ameuawa katika mapigano kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria ameongeza kuwa, wapiganaji kadhaa wa Boko Haram wameuawa pia katika mapigano yanayoendelea kati ya jeshi na wanamgambo hao.

Wakati huo huo taarifa kutoka Nigeria zinasema kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuukomboa msitu wa Sambisa ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya kundi la kigaidi la Boko Haram.

Msitu wa Sambisa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria uko umbali wa karibu kilomita 100 kutoka Chibok mji ambao mnamo mwaka mmoja uliopita kundi la Boko Haram liliteka nyara zaidi ya wasichana 200 wa shule na kuwapeleka kusikojulikana.

Hayo yanajiri katika hali ambayo operesheni ya pamoja ya vikosi vya Nigeria, Chad, Cameroon na Niger dhidi ya Boko Haram inaendelea huku kukiwa na taarifa kwamba, imekuwa na mafanikio

ZITTO KABWE NI BALAAA: HIZI NI PICHA 10 ZA MKUTANO WA ACT MKOANI TABORA....WATU WALIJAA KUPITA MAELEZO



Kiongozi  Mkuu  wa  Chama  cha  ACT-Wazalendo  akiwahutubia  mamia  ya  Wananchi  Mkoani  Tabora  Jana. 






EX WA SHAMSA FORD AMMWAGIA SIFA EX WA NAY WA MITEGO, SIWEMA

EX WA SHAMSA FORD AMMWAGIA SIFA EX WA NAY WA MITEGO, SIWEMA
siwema-3












Mume wa Shamsa Ford, Dicky ametumia ukurasa wake wa Instagram kumwagia sifa aliyekuwa mpenzi wa Nay Wa Mitego, Siwema. 

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mke wa Dicky, muigizaji Shamsa Ford kuonekana kwenye picha zilizosambaa mtandaoni akimbusu Nay wa Mitego!

Hivyo anachokifanya Dicky kwa sasa ni kulipiza kisasi kwa Nay aliyemchukulia mke wake!

Hizi ni picha alizoweka kwenye Instagram na kumwagia sifa Siwema.
siwema-2
siwema-1
siwema-4