MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete Ijumaa alifanyiwa sherehe za kijadi za kabila la Kikwere kijijini kwao Msoga, kwa mujibu wa mila za hapo.
Sherehe
hizo, ambazo ziliendana na kukabidhiwa vitu mbalimbali vya kijadi kwa
ajili ya matumizi ya nyumbani, ni jadi ya Wakwere ambapo mtu baada ya
kupata uongozi hutambikiwa na kukaribishwa rasmi kwenye kundi la wazee
wa kijiji.
Baadhi
ya vitu alivyoakabidhiwa na mzee wa kabila hilo Zaidi Rufunga ni pamoja
na kitanda cha kamba, msuli, kigoda na kinu pamoja na vitu mbalimbali.
Sherehe hizo za kijadi ziliamabatana na ngoma ya Kikwere na ulaji wa
chakula kiitwacho Bambiko ambacho hutumiwa na kabila hilo.
Mzee
Zaidi Rufunga kulia akimkabidhi vyungu mbunge wa Jimbo la Chalinze
wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete wakati wa sherehe za
jadi za kumkaribisha nyumbani zilizofanyika juzi kijiji cha Msoga.
Kulia
mzee Zaidi Rufunga akimuelekeza jambo kabla ya kula chakula cha jadi
cha kabila la Wakwere kiitwacho Bambiko wakati wa sherehe za jadi za
kumkaribisha nyumbani Ridhiwani Kikwete zilizofanyika juzi kijijini
hapo.
Baadhi
ya akina mama waliohudhuria sherehe za jadi za kumkaribisha mbunge wa
Jimbo la Chalinze Ridhiwani KIkwete zilizofanyika Ijumaa kijijini Msoga.
0 comments:
Post a Comment