Katika hali ya kawaida, kila mtu anapofikiria suala la kutafuta mpenzi kwa mwanaumelazima ataangalia msichana mrembo, mwenye muonekano mzuri huku suala la tabia likiwa halipewi umuhimu sana.Hata
kwa wanawake nao huwa wanaangalia wanaume ‘handsome’ ambao hata wakiwa
wanatembea pamoja mtaani watavuta macho ya watu na kusifiwa.
Mimi
sidhani kama wanaoangalia vigezo hivyo wanakosea hasa kama wanatafuta
wapenzi na wachumba watakaotengeneza njia ya kuelekea kwenye ndoa.
Naomba
katika hili nieleweke kwamba, suala la muonekano wa mtu si kigezo tosha
cha kumruhusu awe sehemu yako katika maisha ya ndoa. Wapo ambao ni
‘handsome’ na warembo lakini kiukweli hawastahili kupewa nafasi ya
kuingia nao kwenye ndoa.
Tatizo la wanaume ‘handsome’
Utafiti
nilioufanya ambao siyo rasmi unaonesha kwamba, ni wachache sana waliooa
wanawake wazuri na wakaishi muda mrefu tena kwa furaha na amani.
Tunachotakiwa
kujua katika hili ni kwamba, kuna baadhi ya wanaume ambao wanajijua
wanapendwa sana na wanawake kutokana na muonekano wao. Kwamba ni warefu,
ni watu wa mazoezi, wana sura nzuri na sifa nyinginezo.
Wenye
sifa hizi ni chaguo la wanawake wengi. Kutokana na hilo sasa, wapo
ambao wana kaulimbukeni f’lani ka’ kushindwa kutulia na mwanamke mmoja.
Wanaweza kuingia kwenye ndoa lakini bado wakashawishika kutembea na
wanawake wengine kwa kuahidiwa fedha na vitu vingine.Mbaya
zaidi, wanaume wa dizaini hii watakuwa wanajisahau kwamba nyumbani wana
wake zao ambao wamewakabidhi mioyo yao na hawatarajii kusalitiwa.Hapo
ndipo tatizo litakapoanzia na kumfanya hata mke mwenyewe ajute kuingia
kwenye ndoa na mwanaume ‘handsome’. Sisemi kwamba wanaume ‘handsome’
wote ni tatizo kwenye ndoa, la hasha!
Wapo
ambao ni watulivu, wasio viruka njia, kwamba wakipenda mmoja wamependa
na hata wakishawishiwa na wengine, husimamia hisia zao na kuangalia
heshima yao mbele ya jamii.
Tatizo ni kwamba, kuna ambao kwa muonekano huwezi kuwajua lakini ukishakubali ndoa utashangaa usumbufu utakaopata.
Utaona
mumeo ana marafiki wengi wa kike na ukimuuliza anasema ni marafiki tu.
Mara utamuona anabadilisha magari na ukifuatilia utaambiwa ni magari ya
mwanamke f’lani mwenye nazo. Hapo sasa ndipo utajua kwamba kumbe
hujapenda peke yako, wapo wengine waliopenda na wakapewa nafasi kutokana
na ushawishi wao.
Ndiyo
maana nasema kuolewa na mwanaume ‘handsome’ tena ambaye ni limbukeni,
utapata tabu sana. Utaambulia ile sifa tu ya kwamba umeolewa na mwanaume
mzuri lakini kumbe hafai kuitwa mume!
Wasichana warembo nao!
Jaribu
kuchunguza utabaini kuwa, asilimia kubwa ya wanaume wanaoteswa na ndoa
zao, wameoa wasichana warembo lakini wasiojua thamani ya ndoa. Watakuwa
wanaona sifa kuolewa lakini bado hawajui namna ya kuzitunza ndoa zao.
Watakuwa
warahisi kushawishiwa na wanaume wakware na wakati mwingine wakiona
wanatongozwa sana kutokana na uzuri wao, wanavimba vichwa.Wanakuwa si
watulivu kwenye ndoa zao, siyo watiifu kwa waume zao na wanafanya hivyo
wakiamini kwamba hata wakiachika, watapata wanaume wengine wa kuwaoa.
Ndiyo
maana huwa nasema mara kwa mara kwamba, ukitaka kuoa ni lazima uangalie
mwanamke mzuri unayemuona wewe. Lakini usiishie hapo, angalia na tabia
zake ili usije ukaingia kwa mtu ambaye hawezi kukupa furaha ya ndoa
uliyotarajia.
Katika
hili naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, ukitaka kuingia kwenye ndoa
epuka sana kuangalia muonekano wa mtu. Tukijichanganya macho
yatatuingiza mkenge!Unaweza kumuona msichana mzuri, mwenye figa na sura
ya kuvutia au mwanaume ‘handsome’, mwenye sifa zote za kupendwa na kila
mwanamke lakini kumbe linapokuja suala la ndoa, hamna kitu!
Ni
suala la wewe kuwa makini sana hasa pale unapotafuta mpenzi au mchumba!
Achana na ile tabia ya kutafuta sifa kwamba eti ‘kapo’ yenu inavutia,
swali ni je, anaiheshimu ndoa na siyo macho juujuu?
0 comments:
Post a Comment