“Ni
mwaka mzima umepita tangu tumalize kazi yetu. Wajumbe wa tume
hawakwenda kufanya kazi ya kuandaa rasimu kwa ajili ya kutafuta fedha.”
Serikali
imeanza kulipa kiinua mgongo kwa wajumbe wa iliyokuwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Wariona na jumla ya
Sh640 milioni zitalipwa kwa watu 32.
Tume
hiyo, ambayo ilifanya kazi ya kukusanya maoni na kuandika rasimu mbili
za Katiba kwa miaka miwili, iliwasilisha ripoti yake kwenye Bunge
Maalumu la Katiba mwezi Machi mwaka jana, ikiwa ni kutimiza kifungu cha
31 (1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Rais
Jakaya Kikwete alisema kuwa anafikiria kuwalipa wajumbe wa tume hiyo
aina fulani ya kifuta jasho ambacho kiwango chake atakiamua yeye na kwa
wakati mwafaka na kulingana na rasilimali za Serikali.
Habari
ambazo paparazi imezipata zinasema kuwa wajumbe wa kamati hiyo
wanalipwa Sh20 milioni kila mmoja, tofauti na habari zilizokuwa
zimezagaa kuwa kila mjumbe angelipwa Sh200 milioni. Uchunguzi wa
paparazi umebaini kuwa mbali na wajumbe hao, makamishna wapatao 30 na
viongozi wao wawili kutoka Bara na Visiwani walioshirikiana na tume
kufanya kazi hiyo, wamo kwenye mpango huo, lakini inaonekana baadhi ya
wajumbe hawajaridhika na kiwango hicho.
“Pamoja
na kumshkuru Rais Kikwete kwa kufanikisha malipo yetu ya mafao, bado
naona kiwango tulicholipwa ni kidogo kutokana na ukubwa wa kazi na uzito
wake,” alisema mmoja wa makamishna ambaye aliomba jina lake
lihifadhiwe.
Alisema
kwamba wakati wakisubiri kulipwa mafao yao kwa takriban mwaka, walikuwa
na matumaini makubwa ya kulipwa kiasi cha Sh35 milioni kila mmoja
kutokana na kazi kubwa waliyoifanya.
Hata
hivyo, Jaji Warioba alisema wakati wanakubali kufanya kazi hiyo,
hawakuwa na tamaa ya fedha na kwamba kama kuna malalamiko, basi ni ya
mtu binafsi na siyo tume.
Alisema
Rais alipewa uwezo wa kisheria kupanga na kuamua viwango vya kulipwa
mafao viongozi wa tume hiyo baada ya kukamilisha kazi kwa jinsi
atakavyoona inafaa.
Alisema
kuwa hata barua zao za uteuzi zilisema watakuwa wakilipwa kiasi fulani
wakiwa kazini na wakimaliza kazi, Serikali itawalipa kiinua mgongo kwa
jinsi Rais atakavyoamua.
“Hivi
karibuni Serikali ilinieleza kuwa italipa fedha hiyo na mimi
nikawaeleza wajumbe. Sikuwa nikipata malalamiko kwamba wanategemea kiasi
gani. Wapo ambao walikuwa wamesahau kabisa kuwa kuna malipo hayo,”
alisema.
“Mimi
kama mwenyekiti wao najua wajumbe hawakuwa na tamaa ya fedha na kama
kuna malalamiko yoyote basi ni ya mtu mmoja lakini siyo tume.”
0 comments:
Post a Comment