Dada
huyu pichani jana aliandamwa na kuzomewa na baadhi ya wakazi wa Iringa
Mjini hususan wanaume wakidai kuwa ametembea nusu uchi. Jambo hili
linakanganya; ni nani mwenye mamlaka ya kuamua kama anayetembea
barabarani yu nusu uchi au la? Maana, fasheni siku hizi ziko za aina
mbali mbali.
Dada
huyu amefanya kosa gani? Je, jambo hili lingewezekana kutokea kwenye
miji kama Dar ambako si tu huonekana wanaume kwa wanawake wenye kuvaa
fasheni mbali mbali za Kimagharibi?
Mbona
hawazomewi dada zetu wenye kucheza shoo kwenye steji za muziki wakiwa
na ' vichupi'? Na wanaume wenye kutembea vifua wazi na kuvaa suruali
nusu matako tuwafanyeje?
Dada
aliyezomewa na wanaume ana haki ya kudai kuwa amedhalilishwa kijinsia
kama akipeleka kwa hakimu ushahidi wa picha hizo. Katika hili '
Mwenyekiti' wenu naweza ' KujiTunduLisssu' na kusimama mahakamani
kumtetea dada yangu huyu. Na namini atashinda na kulipwa fidia!
Na nyie mmesimamia wapi kwenye mkanganyiko huu?
0 comments:
Post a Comment