Diamond: Aliyenifundisha Kuongea Kiingereza ni Penny, sio Wema Sepetu | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

Diamond: Aliyenifundisha Kuongea Kiingereza ni Penny, sio Wema Sepetu



Wakati  kila mtu akiamini mwalimu wake wa lugha ya Kiingereza ni Wema Sepetu ‘Madam’ staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kudai aliyemfundisha lugha hiyo ni aliyekuwa mpenzi wake, Peniel Mungilwa.
 
Diamond aliwataka watu wote waliokuwa wakiamini Wema ndiye mwalimu wake wa ung’eng’e wafute imani hiyo kwani Penny ndiye mpango mzima.

“Ujue kila mtu huwa ana hisia zake na wengi wamekuwa wakiishi kwa hisia, nimekuwa nikiambiwa kuwa Wema ana mchango mkubwa katika uzungumzaji wangu wa Kiingereza jambo ambalo si kweli, aliyenifundisha lugha hiyo kwa sehemu kubwa ni Penny maana aliniletea hadi mwalimu ingawa nilikuwa nikimlipa mwenyewe,” alisema Diamond.
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment