Akizungumzia ishu hiyo Tunda Man amesema anachohisi alimkosea Matonya ni kusema kama alimtungia nyimbo lakini hataki tena kuzungumzia swala hilo na leo ndio itakuwa mara ya mwisho kuzungumzia jambo hilo na kuomba msamaha kwa yote yaliyotokea na kuanzia sasa hana tatizo na Matonya ambae hawajaonana toka mwaka 2007.
Matonya amesema kuwa Tunda Man ni mdogo wake ambae wamekutana vizuri na walikuwa wanaishi vizuri lakini alipata wasiwasi baada ya kuona kila siku kunakuwa na maneno, lakini yeye binafsi anampenda Tunda Man na hata familia yake, ila hakupenda maneno aliyokuwa anazungumza lakini yeye kama kaka ameamua kumsamehe kwa yote aliyomkosea na leo wataenda studio kufanya collabo.
Kusikiliza story yote ya Hekaheka bonyeza play hapa chini.
0 comments:
Post a Comment