G Nako na ishu ya kutoza HELA kwenye collabo, kuingia kwenye uigizaji.. | HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz

G Nako na ishu ya kutoza HELA kwenye collabo, kuingia kwenye uigizaji..

.
.
Rapper wa kundi la Weusi, G Nako amezungumzia kuhusu na kuendelea kuwatoza fedha wasanii wanaomshirikisha katika nyimbo zao pamoja na ishu ya kuingia kwenye filamu.
Uamuzi wa kuwatoza fedha wasanii katika nyimbo zao wanazonishirikisha bado unaendelea ,unajua muziki wetu unapanuka na watu wengi wanaujua kwa hiyo lazima sasa hivi tuwe katika level za kimataifa..  japokuwa bado katika stage ya kuwaweka watu sawa wasiwe wageni sana na hiki kitu kwa sababu unaweza ukatoka kama msanii kwenda nchi nyingine ukashangaa lakini sio kitu cha kushangaa.. ni kitu cha kawaida kabisa..“– G Nako
Mbali na kutoza fedha wasanii katika nyimbo anazoshirikishwa, kagusia pia kuhusiana na kuingia kwenye uigizaji; “Unajua kwenye sanaa kuna mahusiano  kati ya vitu viwili ambazo ni muziki na filamu kwa hiyo mashabiki wasishangee kuniona kwenye TV. Kuna short clips nimeigiza kwenye hiyo series ila bado haijatoka, tuko kwenye maandalizi ya kuelekea kumalizia“–alisema G Nako.
SHARE

Unknown

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment