HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz - POLITICS HABARI MATUKIO TEKNOLOJIA NDANI NA NJE YA Tz: POLITICS - All Post
Showing posts with label POLITICS. Show all posts
Showing posts with label POLITICS. Show all posts

I NEVER GET A NAMES OF THOSE SENTENCED TO DEATH FOR KILLING ALBINO - JK

I NEVER GET A NAMES OF THOSE SENTENCED TO DEATH FOR KILLING ALBINO - JK
President of the United Republic of Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete has said that he brought the names of 16 people who were sentenced to death for the murder of albino country because legal journey these names passed on him is long.
President Kikwete made the remarks yesterday, Sunday, April 12, 2015 when he spoke at a special rite of ordination and consecration of a bishop Liberatus Sangu that Rev. Father Bishop of the Catholic Church of Shinyanga.
Speaking in worship that took place at the Cathedral of the Mother Merciful, Ngokolo, in Shinyanga and the presence of many leaders of the church, including the archbishops, bishops and bishops assistants 38, the President took the opportunity to respond to allegations that his government not taking adequate measures to cope with albinism and also elaborate on the pressure that is made by some non-governmental organizations (NGO's) yakimtaka President sign of letting them be hanged.
President Kikwete told the religious leaders: "I have a special request for you clergy. Allow me to help us educate the community to iachane and superstitious beliefs. Elderly people are being killed just because of having red eyes and extreme ignorance that causes fellow Tanzanians with albinism (albinos) being hunted and killed quite brutally. "
"I beg you, help each other extremely religious leaders in stopping this massive ignorance to awareness to your disciples, to know that elderly people have red eyes because of using cow dung cooking for a long time and that link is not ready for albino bring any wealth," The President told the religious leaders.
Regarding allegations that his government is not doing enough to tackle measures albinism, President Kikwete told the leaders: "Many suspects arrested Tumewatia albinism. 16 people have already been sentenced to death and others are waiting ... their cases continue to be heard. There are words words, but personally as President I brought the names of those people. "
He added: "We must understand how our system works to give rights especially in the area of ​​execution, or execute. It is a long chain. In the case of those sentenced to death, the first appeal is mandatory and not a matter of choice or requirement of the condemned. Second, we finished and appeals must Exemption Committee (Committee on Prerogative of Mercy), and to work. So it is a long process a little bit. "
Rev. Bishop Sangu, who was appointed by the Holy Father Bishop Francesco February 2, this year, 2015, has taken the place of the late Bishop Aloysius Balina who died November 6, 2012.
At the time of his appointment, Mosinyori Sangu was working at the Department of Spreading the Gospel world at the headquarters of the Catholic Church, the Vatican, where he worked for eight years

Kumbe Charles Hillary kaondoka BBC na kuamua kurudi nyumbani?

Kumbe Charles Hillary kaondoka BBC na kuamua kurudi nyumbani?
 Chaz 1
Miongoni mwa watu ambao sauti zao zimesikika sana kupitia BBC London, ni Mtangazaji Mtanzania Charles Hillary aliyewahi kusikika sana hata kupitia Radio One pia.
Charles Hillary sasa anarudi nyumbani Tanzania na kujiunga na kituo cha Televisheni cha Azam ambapo mhariri wa BBC Afrika Dar es salaam Solomon Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary.
Naibu Mtendaji mkuu wa Azam Tido Muhando alithibitisha Hillary kutarajiwa kujiunga na Azam Media akiwa na historia nzuri kwenye vyombo vya habari kuanzia alipoanza mwaka 1994 Radio one na kabla ya hapo alitokea radio Deutsch Welle na mwaka 2006 alijiunga na BBC.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza

Hatimaye Zitto Kabwe Alitema Jimbo Lake la Kigoma Kaskazini...Ajipanga Kwa Majukumu Mazito.. hotuba yake nzima hii hapa

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewaaga rasmi wananchi wa jimbo hilo huku akiwataka wananchi hao kutosononeka kwa uamuzi wake wa kutoendelea kugombea ubunge wa jimbo hilo, bali wamwombee na kumuunga mkono katika kila uamuzi atakaouchukua.

Zitto aliwaaga wananchi hao kupitia mkutano wa hadhara mjini Kigoma uliorushwa moja kwa moja na Kituo cha Radio cha Clouds, ambapo alisema, kipindi cha miaka 10 kinatosha kwa yeye kuwa mbunge wa jimbo hilo hivyo kwa sasa ni vyema kijiti akapewa mtu mwingine, ili yeye aweze kusonga mbele katika kuwatumikia Watanzania kwa nafasi kubwa zaidi.
  Hii  ni  Hotuba  Yake  Aliyoitoa  March 15, 2015
Mwanamapinduzi na Rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara alisema kuwa ili kuleta mabadiliko ya kimapinduzi ni lazima kuwa na hali fulani ya uendawazimu.
  Ila tusiufikirie uendawazimu huu wa kuokota makopo bali ule ukichaa mzuri wa kuamini katika mambo au misingi fulani na kuisimamia kwa dhati pamoja na changamoto nyingi.
  Kwa kuamini kwa dhati katika mabadiliko haya na kutaka kuboresha maisha ya wanakigoma, mwaka 2005 nilikuja kwenu kuwaomba ridhaa ya kuwatumikia kama mwakilishi wenu Dodoma. Nikiwa na umri wa miaka 29 tu.
  Labda ulikuwa ni msukumo wa matumaini yangu makubwa yanayoambatana na ujana yaliyowashawishi, kwani mliniamini na kunipa kazi hiyo ya heshima kubwa ya kuwawakilisha.
  Mwaka 2010 mliniamini tena, naamini kutokana na utekelezaji wangu mzuri wa kazi na mafanikio tuliyoyaweza kuyapata katika jimbo letu.
  Hivyo kwa miaka kumi tumekuwa bega kwa bega katika safari hii ya pamoja ya kujenga na kuiendeleza jimbo letu, na leo nimekuja kuwashukuru kwa fursa mliyonipa kwani safari yetu inafikia mwisho. Fursa mliyonipa ni ya kipekee kwani ilikuwa fursa si tu ya kuwatumikia ninyi bali kulitumikia Taifa langu.
  Katika miaka kumi hii kuna mambo makubwa tumeyafanya pamoja na kufanikiwa; na kuna mambo ambayo hatukuweza kuyafanya. Kwa yale ambayo hatukuweza kuyafanya naomba radhi. Kwa yale ambayo tumeweza kuyafanya naomba kuwapongeza sana kwa kufanikisha. Kwani kama Mwalimu Nyerere alivyotuambia kuhusu Uhuru na Maendeleo:
  “Uongozi ni kuongea na kujadili na wananchi, kuwaelewesha na kuwashawishi. Uongozi ni kufanya kazi pamoja na wananchi na kuonyesha kwa vitendo mnachotaka kufikia. Uongozi ni kuwa mmoja wa wananchi na kutambua kuwa mko sawa…. Wananchi hawawezi kuendelezwa bali wanajiendeleza.” Na ndivyo tulivyofanya kwa miaka kumi, na kwa ushirikiano wenu tumeweza kufanikisha miradi mikubwa katika Jimbo letu.
  Mwaka 2005 tulikuwa hatuna barabara ya lami hata moja. Leo hii, ninapoongea nanyi tuna barabara za lami zenye zaidi ya kilomita 100 kuunganisha Jimbo letu na majimbo mengine kwa pande zote za nchi kavu. Vilevile tuna mradi mkubwa wa kuunganisha vijiji vya ufukweni mwa Ziwa Tanganyika kwa barabara.
  Kiujumla kwa mkoa wa Kigoma tumefanikiwa kumaliza daraja la Malagarasi na hivyo kuunganisha mkoa wetu na mkoa wa Tabora kwa lami jambo ambalo lilikuwa kilio chetu cha muda mrefu sana tokea enzi na enzi. Muhimu zaidi ni kuwa barabara hizi zinatumika na wananchi, wafanyabiashara na wakulima ili kuwasiliana, kufanya biashara na kupanua masoko.
  Tumefanikiwa kuongeza huduma ya Nishati ya Umeme kwa kuunganisha vijiji zaidi ya 16 hivi sasa. Changamoto kubwa iliyobakia mkoani kwetu ni uzalishaji mdogo wa umeme na wenye gharama kubwa sana. Suluhisho la kudumu ni kufanikisha mradi wa Malagarasi wenye uwezo wa kuzalisha 44MW ambao utakuwa nafuu na kuwezesha pia kusambaza umeme mikoa jirani ya Katavi na Tabora, na hata kuuza nchi jirani ya Burundi.
  Viongozi wa kisiasa wa mkoa wa Kigoma watakaoingia kwenye uongozi baada ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka 2015 hawana budi kuweka kipaumbele kikubwa kwa mradi huu. Bila ya umeme wa uhakika na nafuu hatuwezi kupiga hatua ya kuongeza thamani ya mazao yetu kwa kujenga viwanda vya usindikaji na kuongeza ajira ya vijana wetu.
  Tumefanikiwa kuanza miradi ya Bandari na Soko kubwa kijiji cha Kagunga. Lengo likiwa ni kukuza biashara ya bidhaa kati yetu na nchi ya Burundi. Kigoma ni mji wa biashara kiasili na biashara ilichukua nafasi kubwa ya uchumi wa mkoa huu kwa miaka mingi sana. Kuimarishwa kwa miundombinu ya Biashara ni sehemu ya miradi ya kimkakati katika kuuweka mkoa kuchukua nafasi yake ya kiuchumi katika nchi yetu.
  Katika muktadha huo ndio maana tunaendelea na miradi ya Bandari Kibirizi na Bandari ya Nchi Kavu Katosho. Ndio maana tunaendelea na mradi wa Kituo cha Usafirishaji Mwandiga ( Mwandiga International Transportation Terminal ) na eneo maalumu la kiuchumi Ujiji. Haya yote tuliyaanzisha kwa pamoja nanyi ili kuhakikisha kuwa uchumi wetu unazalisha ajira kwa watu.
  Tumefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi wa sekondari kwa kuwa na shule katika kata na baadhi ya kata tumejenga shule kila kijiji. Hata hivyo, tuna changamoto kubwa sana ya ubora wa elimu katika mkoa wetu. Katika jimbo la Kigoma Kaskazini zaidi ya 90% ya watahiniwa wa Kidato cha Nne wanapata madaraja ya mawili ya chini, wakati ule daraja la nne na daraja la sifuri.
  Tumeanzisha mradi wa majaribio ya kutoa motisha kwa Walimu ili kuona namna bora zaidi ya kuhakikisha elimu inaboreshwa. Shirika la Twaweza linaendesha mradi mkubwa wa motisha kwa walimu na baada ya mwaka huu tutakuwa tumejifunza njia bora za kuongeza ubora wa elimu kwa watoto wetu. Bila Elimu bora miradi yote niliyoeleza hapo awali haina maana yeyote.
  Serikali imetoa Sera mpya ya Elimu, ni wajibu wetu kuona namna ya kuitekeleza katika ngazi yetu ili kupata mafanikio. Hata hivyo, uongozi wa kisiasa utakaoingia baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu hauna budi kujielekeza vya kutosha katika elimu ya ufundi ili kujenga stadi za kazi kwa vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.
  Tumefanikiwa kupanua huduma ya Afya kwa kuboresha Zahanati zetu chache zilizokuwepo na kujenga zahanati kadhaa mpya na miradi ya vituo vya afya vya Mahembe na Nyarubanda. 
  Hata hivyo nasisitiza sana umuhimu wa kinga kuliko tiba kwani gharama za afya zimekuwa kubwa sana. Ndiyo maana tulipojadili hili suala, ilionekana kuwa suluhisho linatakiwa lipatikane kwa kufanya kile ambacho hatujawahi kufanya ili kuleta maendeleo ya kweli.
  Na mniruhusu hapa kunukuu wosia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alipotuasi kuwa “Maendeleo ni maendeleo ya watu. Barabara, Majengo, kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao na masuala mengi kama haya si maendeleo, bali ni vitendea kazi tu vya maendeleo” 
  Ndiyo maana kulikuwa na umuhimu wa kutafuta njia mpya na mbadala kuboresha maisha ya mwananchi, hususan kwa upande wa afya. Uthibitisho wa ubunifu wetu ni kuwa katika kipindi hiki cha miaka 10 tumefanikiwa kuanzisha hifadhi ya jamii kwa wakulima.
  Tulianza na Ushirika wa Wakulima wa Kahawa wa RUMAKU ambapo wananchi walijiunga na NSSF na hivyo kupata mikopo ya muda mfupi, huduma za afya bure na kujiwekea akiba kwa ajili ya mafao ya muda mrefu.
   Mafanikio makubwa yaliyopatikana yamewezesha wazo hili kusambaa nchi nzima na hivi sasa wakulima wa Korosho, Chai, Pamba, Tumbaku wanafuata nyayo za Wakulima wa Ushirika wa RUMAKU.
  Hapa Kigoma wazo hili sasa linatekelezwa kwa wavuvi wa mwambao mwa Ziwa Tanganyika. Ndoto yetu ni wananchi zaidi ya theluthi moja kwenye nguvu kazi wawe na Hifadhi ya Jamii. 
  Natoa wito kwa wananchi wengine wenye uwezo wa kuchangia hifadhi ya jamii wajiunge na vikundi vya ushirika na kuchangia ili kufaidika na mafao ya muda mrefu kama pensheni lakini pia yale ya muda mfupi kama bima ya afya, mikopo kupitia SACCOS na mengine yatakayoanzishwa kama bima ya mazao.
  Tumefanikiwa kujenga heshima ya watu wa Kigoma hapa nchini. Hivi sasa watu wa Kigoma tunatembea kifua mbele bila woga kuliko hapo awali. Kujiamini na kushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano ni wajibu wetu kama raia. Changamoto za kujiona raia wa daraja la pili zimeondoka na zinaendelea kutokomezwa. 
  Juhudi zetu ni silaha kubwa katika kuhakikisha tunakuwa sehemu ya Jamhuri yetu katika kila Nyanja za maisha yetu. Nafurahi kupata fursa ya kushiriki nanyi katika kujenga heshima hiyo ya Mkoa wetu. Nitaendelea kushiriki katika kudumisha heshima hiyo.
  Nimejifunza mengi sana katika safari hii ya utumishi kwenu. Kama nilivyosema hapo awali, mliamua kufanya kile kisichozoeleka katika siasa ya nchi yetu kwa kunipa jukumu hili nikiwa kijana mdogo.
   Naamini kuwa ule ukichaa wangu mzuri wa kusimamia misingi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wangu na kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia nimezipigania. Na katika safari hii nimejenga marafiki wengi sana na pengine hata maadui ingawa hao ni wachache. Lakini haijalishi kwani mi binafsi sina uhasama na binadamu mwenzangu.
  Katika utumishi wangu kwenu, bungeni nimejifunza namna nchi yetu inaendeshwa. Katika kujifunza huko kuna mambo kadhaa nimefanya ya kujivunia na mengine ni makosa. Mliniruhusu kufanya makosa na kuyarekebisha makosa hayo kwa hiyo kukomaa zaidi.
  Shukrani za dhati ziwaendee wazee wangu ambao mliniongoza mpaka hapa tulipofika na kunishauri hata kunionya pale palipohitajika. Kwa ujumla nimejifunza kuwa mzalendo zaidi kwa nchi yangu na kuwatumikia watu wa nchi hii.
   Ndio maana hamkunisikia tu kutetea watu wa Kigoma pekee, bali watu maeneo mengine ya nchi yetu na makundi mbalimbali ya kijamii kama Wakulima, Wafanyakazi, Wasanii, Wavuvi, Wana michezo na wana habari.
  Katika safari hii ya miaka 10 kuna watu nimewafurahisha na kuna watu nimewaudhi. Kwa wale niliowaudhi ninaomba radhi. Kwa wale niliowafurahisha ninaomba wasiache kuniongoza na kunishauri kila wakati.
 Haikuwa safari rahisi na sikutegemea iwe rahisi. Kiuhalisia ilikuwa safari ngumu yenye mafunzo makubwa kwangu. Ilikuwa ni safari yangu kama kiongozi na pia safari yangu binafsi ya kupevuka kifikra na kupata mafunzo kuhusu maisha.
  Ukifika ulikokuwa unakwenda katika safari, unaweza kutathmini mengi kuhusu safari hiyo, lakini mwisho wa siku unatakiwa ujue kama safari hii ilikuwa njema ama la. Ninajivunia safari hii na ninasema kwa dhati kabisa ilikuwa ni safari njema.
  Ni wakati sasa wa kutoa nafasi kwa nguvu mpya kuongoza Jimbo letu. Kushika kijiti pale ninapoishia. Kurekebisha pale nilipokosea. Kuimarisha pale nilipofikia.
  Sitakuwa mbunge wenu baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba lakini nitaendelea kutetea maslahi ya Mkoa wa Kigoma na Taifa letu kwa njia nyingine.
  Sitaacha ule uendawazimu mzuri aliyoizungumzia Thomas Sankara unaoleta maendeleo ya kimapinduzi. Na misingi ni ileile na maadui ni walewale ambao mwasisi wetu Mwalimu Nyerere aliyokuwa anasema tupambane nao, yaani umaskini, ujinga, maradhi na sasa tumeongeza ufisadi.
  Kizazi chetu kina jukumu la kipekee kuendeleza mapambano haya na nitaendelea kuhakikisha tunafanya mapinduzi na kuwa na Taifa lenye misingi madhubuti ya uwajibikaji ili kuondoa kila aina ya ufisadi na kutumia rasilimali za nchi kuondoa umasikini, ujinga na maradhi.
Asanteni sana Kigoma Kaskazini!

Waziri sitta kuwachukulia hatua waliofanya ufisadi katika uagizaji wa mabehewa mabovu TRL


Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema kuwa mabehewa yaliyoingizwa nchini kutokea Kampuni ya M/S Hindusthan Engeneering Industries Limited yapo chini ya kiwango na hivyo wale ambao wamehusika na ukaguzi na kufanya mabehewa hayo yaingizwe nchini watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara alipotembelea Shirika la Reli Nchini (TRL),Sitta alisema serikali ikithibitisha waliokagua na kuleta mabehewa hayo watachukuliwa hatua.“Nchi hii ni masikini hivyo wote waliohusika katika uingizaji wa mabehewa hayo watachukuliwa hatua kutokana na sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kusitisha mkataba  huo na hili nitafuatutilia kwa karibu na bodi ya TRL nimeiagiza kufanya hivyo”alisema Sitta.
Alisema kutokana na kuingizwa kwa mabehewa yasio na ubora,wamezuia kuingia tena kwa mabehewa 124 kutokana na mkataba walioingia nao wa kuleta mabebewa hayo.
Sitta alisema hali ya shirika ni nzuri kutokana mapato yake kuongezeka kutokana na watendaji kujipanga katika uendeshaji wa shirika hilo.  
Waziri wa Uchukuzi,Mh. Samwel Sitta (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo,wakati alipotembelea Shirika la Reli nchini (TRL). kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mh. Charles Tizeba na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Monica Mwamunyange,.
Sehemu ya Wanahabari wakimsikiliza Waziri Sitta (hayupo pichani) wakati alipotembelea Shirika la Reli nchini (TRL) jijini Dar leo

Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe...Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA


Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).

Kauli ya hiyo ya Bunge imekuja siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza kumvua uanachama Zitto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema kutokana na hali hiyo, Zitto bado ni mbunge halali wa Kigoma Kaskazini na kwamba anapaswa kuendelea na shughuli zake kwa mujibu wa sheria.

Dk Thomas Kashililah, amebainisha kuwa endapo Bunge litapata taarifa rasmi ya Chadema kumvua uanachama Zitto, lazima Bunge hilo lifanye kwanza uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ndipo litoe uamuzi.

Pia amesema sakata la mbunge wa Bunge hilo kuvuliwa uanachama na chama chake si la kwanza, kwani tayari kuna mbunge aliyevuliwa uanachama na chama chake lakini Bunge hilo halikumvua uanachama wake baada ya kumaliza uchunguzi wake. Hata hivyo hakumtaja mbunge huyo.

“Utaratibu ulivyo, chama huliandikia Bunge kuhusu kumvua uanachama mbunge na Bunge kabla ya uamuzi wowote hufuatilia kwanza sababu za kuvuliwa uanachama huo, ili kujiridhisha kama zilikuwa halali au la,”alisema Kashililah.

Alisema baada ya hapo Bunge hilo huwasiliana na Msajili wa Vyama vya Siasa ili ofisi hiyo ya msajili iweze kupitia Katiba ya chama husika na kupitia sababu za chama husika zinazoweza kumvua uanachama mwanachama wake na kama kweli zimekiukwa.

“Baada ya suala hilo kupelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa, Spika wa Bunge, hutoa uamuzi baada ya kuchunguza na uamuzi huo, hupelekwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi,” alisisitiza.

Aidha alisisitiza: “Si lazima Spika akubaliane na uamuzi wa kutengua ubunge wa mbunge husika kwani kama haikuwa halali kwa mbunge huyo kuvuliwa uanachama, Spika hubatilisha uamuzi wake wa kumvua ubunge mhusika,” alisema.

Alisema Spika Anne Makinda katika kipindi chake alishawahi kutoa uamuzi wa kubatilisha mbunge fulani kuvuliwa ubunge hata baada ya chama chake kumvua uanachama.

Akizungumzia suala hilo, Zitto, alisema kwa upande wake bado ni mbunge na anaendelea na kazi yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) hadi pale atakapopatiwa taarifa rasmi ya kuvuliwa uanachama na ubunge wake.

“Naendelea na kazi kama vile hakuna kilichotokea, sina taarifa yoyote ya kuvuliwa uanachama wangu wala ubunge, habari hizi nimezisikia kwenye vyombo vya habari, sijaitwa na Mahakama kuambiwa kinachoendelea,” alisema Zitto.

Alisema kwa sasa anaendelea kuongoza kamati hiyo na jana alikutana na menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), leo kamati yake inatarajia kukutana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), pia watakutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwanasheria Mkuu kuhusu mapato ya akaunti za madini.

Aidha alisema pamoja na kuendelea kama kawaida na shughuli zake za kibunge bungeni, pia anatarajia kesho kwenda Kigoma kwa ajili ya shughuli za maendeleo jimboni kwake, kabla ya kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza rasmi Machi 17, mwaka huu.

Alisema kwa upande wake, anachukulia suala hilo kama changamoto ambayo inazidi kumkuza na kumkomaza katika medani za siasa nchini na duniani kote.

Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema chama hicho kinajitahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu zote, ikiwemo kuandaa na kuiwasilisha wakati wowote barua inayomvua uanachama Zitto, ili suala hilo lifanyiwe uamuzi mapema.

“Kwa sasa suala hili la Zitto limewaingia Watanzania wengi, sasa sisi tunataka tulifanyie kazi mapema, ili uamuzi ufanywe mapema na suala hili liishe. Kuna mambo mengi ya maana yanahitaji kujadiliwa kitaifa kama vile masuala ya uandikishaji katika Daftari la Wapiga kura kwa mfumo wa BVR,”alisema.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye juzi alitangaza kuwa chama hicho kimemvua uanachama mbunge huyo, jana alimwambia mwandishi kuwa, jopo la wanasheria wa chama hicho litaifikisha taarifa ya Zitto kuvuliwa uanachama kwa Kamati Kuu ya chama ifikapo Mei, mwaka huu.

Alisema, "Kutokana na utaratibu uliopangwa wa Kamati Kuu kukutana kila baada ya miezi mitatu, suala la Zitto litasubiri kikao kingine cha kawaida cha kamati hiyo kitakachokaa mwezi Mei. Kikao kilichopita kilikaa Februari mwaka huu".

Kwa maelezo ya Lissu, baada ya hapo ndipo wataiandikia barua Tume ya Uchaguzi (NEC) kuijulisha kuwa Zitto si mwanachama wa chama hicho tena au la

Mwanza nzima hili ndio litakua gorofa refu kuliko yote 2016.

Mwanza nzima hili ndio litakua gorofa refu kuliko yote 2016.
333Mwanza ni moja ya sehemu tatu za Tanzania ambazo huwa nazipenda sana na hata wakati mwingine kuvutiwa kuzitembelea kila ninapopata nafasi.
Mabadiliko ambayo wengi wangependa kuyaona ni jiji hili lilibarikiwa kwa kupewa pia ziwa Victoria, liendelee kupendeza kihalali kutokana na mpangilio unavyohitajika.
2Hili jengo linajengwa maeneo ya Capri Point ambapo ni jengo la Hoteli litakalokuwa na gorofa kumi na tano, ni jengo la hoteli ambayo ni ya Nyota tano itakayokuwa karibu na vyumba mia mbili vya kulala.
3Limeanza kujengwa tangu November 2013 na linatarajiwa kumalizika mwaka 2016 huku gharama ya kulijenga ikiwa ni zaidi ya bilioni 72


Uteuzi wa Paul Makonda Kuwa Mkuu wa Wilaya Wapingwa Kila Kona.....Anatuhumiwa Kumpiga Warioba na Kumtusi Lowassa Hadharani


Makonda ambaye ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM, jina lake limekuwa kubwa hivi karibuni baada ya kutuhumiwa kumpiga  Jaji Warioba wakati wa  mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
 Pia, kujitokeza kwake hadharani kumpinga Edward Lowassa, kuliongeza jina hilo kuwa maarufu.


Wakizungumza na Paparazi kwa nyakati  tofauti, baadhi ya wasomaji wa mtandao huu, wamedai kuwa uteuzi huo wa Rais ni mzuri ila  alikosea kumweka wilaya ya  Kinondoni yenye matatizo chungu mzima ya kiutendaji ikiwemo migogoro ya mipaka, ardhi, wafanyabiashara ndogondogo na mambo mengine ya ndani.

“Tunampongeza Rais kwa kuteua wakuu wapya wa wilaya, ila kwa huyu Paul Makonda kumweka Kinondoni, ameteleza. Hii wilaya inahitaji mtu mwenye uzoefu mkubwa katika uongozi na uadilifu” alisema Sued Musa.

Naye  Albert Chenza  wa  Dar  alikuwa  na  haya ya  kusema: "Ma-DC kama Makonda wapo kwa ajili ya CCM kutetea maslahi ya CCM au wapo kwa ajili ya wananchi kuwasaidia wananchi?
  
"Ikumbukwe DC ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na DSO akiwa katibu wake, sasa mtu kama Makonda ambaye yupo tayari kufanya vurugu yoyote kutetea maslahi ya CCM leo kupewa u-DC wa Kinondoni tutegemee nini uchaguzi mkuu wa Oct 2015?
  
"Ikitegemea kuna mvutano kati ya wapinzani na CCM ambao vyombo vya usalama vinatakiwa kuleta haki na amani, wapinzani wategemee kupata haki au NGUVU zao ndo itakuwa haki yao? Hakika nuru ya amani inafifia Tanzania.
  
"Hii ni kama tupo disco la kukesha ambalo inatolewa CD hii inawekwa ile na zote unahitaji unywe panadol kuzisikiliza." Alisema  Albert  na  kuongeza:

"Ni dhahiri sasa Mzee Warioba na Taasisi ya Mwalimu Nyerere wamemjua adui yao halisi ni nani. Aliyekua mstari wa mbele kumshambulia na kumfanyia fujo Mzee Warioba amepongezwa rasmi  kwa  kupewa  ukuu  wa  wilaya.
  
"Pia imeendelea kujidhihirisha sasa kuwa Ukitaka U-DC wewe mtukane Lowassa kama Nape Nnauye, Mrisho Gambo na Makonda  walivyofanya.
  
"Na pengine atakayekua jasiri vya kutosha na kumchapa angalao vibao viwili usoni anaweza kupata Ukuu wa Mkoa au Ubalozi kabisa"
  
Sailas Kassa Edward  yeye  anamaoni  tofauti  kidogo, na hapa  anaanza  kwa kumpongeza Makonda: "Siku ya jana (juzi) Rais kikwete alifanya uteuzi wa wakuu wa wilaya ambapo moja ya wateule ni paul Makonda. 
  
"Inanishangaza sana kutoka jana(juzi) mpaka leo(jana) watanzania wamekuwa wakilalamika kupitia mitandao ya kijamii wakikosoa uteuzi wa ndgu makonda. 
  
"Mimi binafsi nampongeza kwa nafasi aliyopata nadhani katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania haijampa rais mamlaka ya kuwatenga watu bali kila mtu ana haki ya kuongoza na pia kuongozwa. 
  
"Kwa watanzania itafika hatua kila mtu mwenye intrest za chama cha mapinduzi hamtaki apate nafasi je nani ana haki na nani hana?

"Nimejaribu kuchunguza haya yote yanatoka wapi mpaka makonda anakuwa gumzo mtaani nikagundua kuwa wapenzi wa Edward Lowassa wameumia sana kuona makonda anakuwa mkuu wa wilaya hasa ukizingatia anafichua mbinu na hila za Lowassa na makundi yake.